Home Siasa ANAYEWANIA KITI CHA UBUNGE JIMBO LA MPWAPWA ATOA NENO KWA WENZAKE

ANAYEWANIA KITI CHA UBUNGE JIMBO LA MPWAPWA ATOA NENO KWA WENZAKE

0
NA DOTTO KWILASA, DODOMA.
MUOMBA  ridhaa ya kuteuliwa na chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi ya ubunge Jimbo la Mpwapwa,Mkoani hapa Nyange  Darabu, amewataka watakaoshindwa katika kinyanganyiro hicho kuendelea kumuunga mkono ambaye atateuliwa ili kukipa ushindi wa kishindo chama hicho.
Nyange ameyasema hayo Jana Wilayani Mpwapwa Mkoani hapa Mara baada ya kukamilisha taratibu zote za uchukuaji fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa Jimbo la Mpwapwa kwa tiketi ya CCM.
Akieleza zaidi,mgombea huyo alisema kuna wanachama ambao huishi bila msimamo ambapo hutegemea ushindi na ikitokea wameshindwa huishia kuhama chama na kuhamia vyama vingine.
Alisema yeye kama chama hakitampitisha atamuunga mkono ambaye atakuwa ameteuliwa kwani anaamini siasa sio uadui.
Nyange aliwataka na wagombea wengine kufanya hivyo kama watashindwa Katika kichang’anyiro hicho.
“Tunaishi na wanachama wenye uchu wa madaraka ,wanakuwa Kama pendera fuata upepo yani hawajui uelekeo wao ni upi,lazima tuwekane wazi kuwa Kuna kushinda na kushindwa,”alisema Nyange.
Pamoja na hayo Nyange ambaye kitaaluma ni Afisa elimu wa  Manispaa ya Kigamboni jijini Dar Es Salaam alisema ikiwa chama hicho kitampa ridhaa ya kugombea atashirikiana na watia nia wengine.
“Ikiwa sitapata ridhaa nitaendelea kushikilia msimamo wangu wa kuwa mwanachama mtiifu wa CCM na ntashirikiana na viongozi wengine Katika mapambano ya uchumi wa nchi yangu,”alisistiza.