Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akiwasili katika Ofisi za CCM wilaya ya Dodona kwa ajili ya kuchukua fomu ya kutetea kiti chake cha Ubunge kwa awamu nyingine tena ya miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akiwa amekaa akisikiliza maelekezo ya Katibu Msaidizi CCM wilaya ya Dodoma Bw.Said Ngomboi kabla ya kuchukua fomu ya kutetea kiti chake cha Ubunge kwa awamu nyingine tena ya miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi Fedha Katibu Msaidizi CCM wilaya ya Dodoma Bw.Said Ngomboi kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kutetea kiti chake cha Ubunge kwa awamu nyingine tena ya miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akikabidhiwa fomu ya kutetea kiti chake cha Ubunge kwa awamu nyingine tena ya miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Msaidizi CCM wilaya ya Dodoma Bw.Said Ngomboi .
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akionyesha fomu yake mara baada ya kuchukua fomu ya kutetea kiti chake cha Ubunge kwa awamu nyingine tena ya miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
……………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma.
NAIBU Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi ,Ajira na Wenye Ulemavu Anthony Mavunde amesema kuwa anawiwa kuwatumikia wananchi wa jimbo la Dodoma Mjini hivyo amechukua fomu ya kutetea nafasi yake katika jimbo la Dodoma Mjini ili kuendelea kushirikiana na wananchi hao kama watampa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia.
Mavunde ambaye ni Mbunge aliyemaliza muda wake kwa kuhudumu katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020,amesema anawania nafasi hiyo kwani bado anahitaji kuendelea kuwahudumia wananchi hususan wa Jimbonla Dodoma katika kuwaletea Maendeleo zaidi.
“Miaka mitano iliyopita siku na tarehe kama ya leo nilichukua fomu ya kugombea ubunge Dodoma mjini na ilikuwa ni safari njema, namshukuru Mungu kwa miaka mitano iliyopita “ameeleza Mavunde.
Akizungumzia wingi wa wagombea waliotia nia Jimbo hilo ambao ni 47, Mavunde amesema hiyo ni ishara ya ukuaji wa Demokrasia ndani ya chama chao pamoja utendaji kazi wa Rais Magufuli kuwavutia walio wengi.
Aidha amewashukuru wananchi kwa kushirikiana nao vizuri kuleta maendeleo ya Dodoma,na kuwaeleza kuwa amewataka ,hapo alikuwa anajifunza kuwatumikia sasa ndio naanza kuwatumikia.
Mavunde amesema kuwa dhamira yake ni kuendelea kuiletea heshima Dodoma kama ambavyo ndani ya miaka mitano Jiji hilo limepiga hatua kubwa za kimaendelea ikiwemo kuongoza kwa ukusanyaji wa mapato, kuongoza kwa mtandao wa barabara za lami pamoja na miradi mikubwa ya kimkakati.