Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma, ndg. Elirehema Nassari,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wanachama 33 waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge Jimbo la Dodoma Mjini
……………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wanachama thelathini na tatu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma wamejitokeza katika kuchukua fomu ya kuomba kupitishwa na chama hicho nafasi ya Ubunge Jimbo la Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma, ndg. Elirehema Nassari, amesema mpaka Sasa wanachama waliojitokeza ni thelathini na tatu kati ya hao wanaume 30 na wanawake 3.
“Kwa siku ya jana ikiwa ni siku ya kwanza waliojitokeza wabongea 24 Kati ya hao Wanawake walikuwa wawili, na leo siku ya pili wamejitokeza 9 na kufikia idadi ya wagombea 33 huku zoezi likiendelea” amesema Nassari.
Chama Cha Mapinduzi CCM kilitangaza kuanzia siku ya jana tarehe 14 hadi tahere 17 july ni siku ya wagombea wa Chama hicho kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama hicho.
Ikumbukwe Jimbo la Dodoma Mjini lilikuwa likiongozwa na Mhe. Antony Mavunde, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughurikia kazi ajira na vijana.