Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela(mwenye suti) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bw. Boniphace Maiga Juma aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara Julai 13, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bw. Boniphace Maiga Juma , aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bw. Boniphace Maiga Juma aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Kutoka kushoto aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe ambaye pia alikuwa mkuu wa wilaya ya Handeni, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Toba Nguvila, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Mhe. Simon Chacha wakifuatilia ibada ya mazishi ya Bw. Boniphace Maiga Juma aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Baadhi ya makatibu tawala wa wilaya nchini wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, katika mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya makatibu tawala wa wilaya nchini walioshiriki mazishi ya ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Handeni, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Toba Nguvila wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma ambaye alifariki kwa ajali ya gari Julai 11,2020, baada ya mazishi yake yaliyofanyika kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama mkoani Mara
……………………………………………………………………………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Katibu tawala wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Bw. Boniphace Maiga Juma aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Julai 11, 2020, yaliyofanyika Julai 13, 2020 kijiji cha Lyamisanga wilayani Butiama Mara.
Akitoa salamu za pole Mhe. Shigela amesema amepokea taarifa ya kifo cha Bw. Boniphace Maiga kwa mshtuko na majonzi makubwa kwa kuwa ameondoka wakati ambao taifa linamhitaji na kumtegemea.
“Boniphace alikuwa kiungo kati ya serikali na wananchi, serikali kuu na halmashauri, serikali na taasisi; tangu nianze kufanya kazi na Boniphace sijawahi kumuona amekasirika alikuwa mcheshi na alifanya kazi zake kwa bidii na unyenyekevu mkubwa, niwahakikishie familia kuwa tutakuwa bega kwa bega na ninyi popote mtakapohitaji msaada wetu, ” alisema Shigela.
“Mhe. Rais alivyopata taarifa ya msiba huu ilimsikitisha sana, alinipigia simu alfajiri akiwa na taarifa zote na picha zote za tukio, tunaye Rais anayependa watu wake, kwa hiyo wafiwa muamini Boniphace ametangulia lakini amepanda mbegu ya upendo kwa Watanzania akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli” aliongeza Shigela.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemzungumzia marehemu Boniphace kama rafiki yake na sehemu ya familia yake, huku akiahidi kuendelea kushirikiana na familia ya marehemu( mama mzazi na mke wa marehemu).
“Boniphace alikuwa rafiki yangu na sehemu ya familia hivyo mimi na familia yangu tutaendelea kuwa sehemu ya familia ya Boniphace, watu wa serikali wamezungumza namna watakavyosaidia kama serikali lakini sisi kama familia kwa lile ambalo mtaona mngehitaji msaada kutoka kwangu sisi bado tuko pamoja,” alisema Mtaka.
Akimzungumzia marehemu Boniphace Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe ambeye alifanya naye kazi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni amesema Boniphace alikuwa kijana mchapakazi anayesikiliza na kutekeleza maagizo ya viongozi wake.
“Siku aliyofariki Boniphace ndiyo siku nilikuwa naenda kumkabidhi ofisi Mkuu mpya wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Toba; siku hiyo tulifanya vikao vitatu mfululizo kuanzia asubuhi mpaka jioni na siku hiyo marehemu Boniphace alikuwa na utani mwingi sana, kweli kifo ni fumbo na hakuna anayeweza kuzoea kifo,” alisema Gondwe.
Akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Mhe. Simon Chacha ametoa pole kwa familia ya marehemu na viongozi wote waliofanya kazi na marehemu kwa kuondokewa na mtu ambaye kwa mkoa wa Mara walimuona kama balozi wao kwa utendaji kazi wake uliotukuka.
Marehemu Boniphace Maiga Juma alizaliwa Aprili 17, 1984 ambapo enzi za uhai wake amewahi kuwa mwalimu na mtumishi wa tume ya utumishi wa walimu na baadaye aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mwezi Mei 2018, marehemu ameacha mke na watoto watatu.