********************************
Mwandishi Wetu, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mhe. Dr.Phillis Nyimbi amesema masuala ya usalama na afya kwa wajasiriamali ni muhimu, kwani kutokuzingatia kwake kuweza kuleta athari kwa mfanyakazi na hivyo kutaathiri jamii na taifa kwa ujumla
Mhe. Nyimbi amesema hayo wakati akifungua Semina maalumu kwa wajasirimali wadogo na wakati ,Semina ya usalama na afya yalioyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na SIDO mkoa wa Mwanza, Semina iliyofanyika Jijini Mwanza. Amesema endapo tahadhari haitachukuliwa, itawasababishia madhara makubwa na hivyo kuwa mzigo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu huyo wa Wilaya amengeza na kusema, wakati mwingine ni kutokutilia maananini kwa baadhi ya watu, na kuacha kununua vifaa vya kuwakinga wakati wakiwa kazini na hivyo kuchangia hatari ya kuweza kupata madhara wakati wakiendelea na kazi.
“Lakini pamoja na hayo, tukumbuke kwamba, suala la usalama na afya nijukumu letu sote, magonjwa na
ajali zinazotokea sehemu za kazi, mara nyingi zina athari nyingi sio kwetu tu, bali hata kwa jamii, Vifaa mnavyotumia, wengine mnatumia kemikali katika uzalishaji wa bidhaa zenu, hii kwa kiasi kikubwa zinaweza zikaleta madhara makubwa kwenu nyinyi na hata wale watakaokwenda kutumia endapo hatua madhubuti hazitachukuliwa, madhara yake yanaweza yakawa makubwa sana, hivyo matumizi sahihi ya vifaa kinga ( PPE) katika kazi zenu hayaepukiki. “ Aliongeza Dr. Nyimbi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo,Utafiti,na Takwimu, Ndugu Joshua Matiko, amesema wajasiriamali wanakabiliwa na changamoto mbalimbali na hivyo kuwataka kila wanapokuwa wanafanya shughuli zao wazungumzie masuala ya usalama na afya kabla ya kuanza kazi, ili kubainisha vihatarishi vinavyopatikana kwenye maeneo yao kazi, unajaribu kuzungumza kuna namna ya kuviepuka .
“ Kuna haja ya kuweka mabango yatakayosaidia kutukumbusha masuala ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi, na hivyo kuchukua tahadhari kwenye maeneo yetu ya kazi” alielezea mkurugenzi wa mafunzo,
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo, wamesema semina hiyo imewajengea msingi mzuri wa kuweza kufanya shughuli zao za uzalishaji huku wakichukua tahadhari ya kufanya kazi katika mazingira salama na kulinda afya zaa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi kufungua semina hiyo, Meneja wa SIDO mkoa wa Mwanza Ndugu Bakari Songwe amesema, SIDO kama taasisi wezesheji kwa wajasiriamali amesema waliona umuhimu wakuwashirikisha OSHA ili waweze kutoa semina ya kuwawezesha wajasirimali hao namna bora ya kufanya kazi huku wakizingatia Usalama na Afya wakiwa kazini.
Mafunzo haya yamefanyika katika mkoa wa Dodoma na sasa Mwanza ambayo yanalenga kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo namna bora ya kulinda usalama na afya kwa wadau wao ambao wanamchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.