Home Mchanganyiko WENYE ULEMAVU JITOKEZENI KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI

WENYE ULEMAVU JITOKEZENI KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI

0

NA MWANDISHI WETU

Wito umetolewa kwa watu wanaoishi na ulemavu kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais unaotariwa kufanyika mwezi Octoba mwaka  huu 2020.

Wito huo umetolewa na mtia nia nafasi ya ubunge viti maalumu wanawake kwa tiketi ya  watu wenye ulemavu, Pano Kashu, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro jana. 

Pano alisema kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa kushiriki katika kuchagua na kuchaguliwa sawasawa na watu wengine wasio na ulemavu. 

“ Wenye ulemavu hawana sababu ya kuogopa kuomba nafasi za kuchaguliwa katika uchaguzi  mkuu ulio mbele yetu. Ni haki yao na wajibu wao kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kuomba nafasi mbali mbali ikiwemo udiwani na ubunge kwa kuwa wapo wenye ulemavu ambao wana uwezo mkubwa wa kuongoza sawasawa na hata kuwazidi wasio na ulemavu, ni haki yao kushiriki uchaguzi.” Alisema Pano.

 Pano aliongeza kusema kuwa upo mtazamo hasi wa jamii kuwa watu wenye ulemavu hawawezi kuwa viongozi wazuri. Anasema kuwa mtazamo huo ni mbaya na umepitwa na wakati na ni vema jamii ikaachana nao.

“ Ulemavu sio kushindwa. Mtu mwenye ulemavu akipewa fursa anaweza sawasawa na mtu asiye na ulemavu na hata kuzidi. Baadhi ya wana jamii huwa inawatazama watu wenye ulemavu kama watu wasioweza, jambo ambalo sio la kweli. Ukweli ni kwamba watu wenye ulemavu wanauwezo mkubwa wa kuongoza na wamejaaliwa vipaji vingi ikiwemo vya uongozi isipokuwa mtazamo wa jamii unafinyaza na kudumaza vipaji hivyo”. Alisema Pano. A

 Pano aliongeza kusema kuwa ni matarajio yake kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na haki na utatoa fursa sawa kwa watu wenye ulemavu ambao wataomba kuchaguliwa sawasawa na watu wengine.

“ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ni Rais wa wanyonge wakiwemo walemavu. Ninaamini kuwa uchaguzi wa mwaka huu wanyonge  hasa watu wenye ulemavu watapata fursa ya kuchagua na kuchaguliwa pasipo upendeleo wala unyanyapaa. Anasema.

 Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Morogoro, Oscar Changala, akizungumza kuhusu ushiriki  wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, alisema kuwa shirikisho limejipanga kutoa elimu  na hamasa kwa  kundi hilo ili waweze kushirika kikamilifu katika kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbali mbali. Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Morogoro, Oscar Changala, akizungumza kuhusu ushiriki  wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, alisema kuwa shirikisho limejipanga kutoa elimu  na hamasa kwa  kundi hilo ili waweze kushirika kikamilifu katika kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbali mbali.