Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja(katikati), akichora ramani chini ikiwa ni kutoa maelekezo kwa wasimizi na mkandarasi anayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika Vijiji vilivyopo pembezoni mwa Mji ( Peri Urban) alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika wilaya ya kisarawe mkoani Pwani, julai 11,2020.
Moja ya nyumba zilizopo katika maeneo yatapitiwa na Mradi wa Kusambaza Umeme katika Vijiji vilivyopo pembezoni mwa Mji (Peri Urban) katika Kijiji cha Vilabwa ikiwa tayari imetandazwa nyaya ikisubiri kuunganishwa na umeme. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika wilaya ya kisarawe mkoani Pwani, julai 11,2020.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja(kushoto),akifurahia jambo na mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mhaga, Ally Zolila kinachopitiwa na Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika Vijiji vilivyopembezoni mwa Mji( Peri Urbani) Naibu Katibu Mkuu huyo alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika Wilaya ya Kisarawe mkoaniPwani, Julai 11,2020.
Kamera ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati ilimmulika kijana Amos Malima, Mkazi wa Kijiji cha Vilabwa aliyekuwa akijaza mafuta aina ya petroli katika chumba ndogo zilizoisha maji kutoka katika Galoni kubwa ililoisha mafuta ya kupikia,uwekaji wa mafuta ya petoli katika mazingira yasiyo salama ni hatari kwakuwa yanaweza kusababisha ajali ya moto wakati wowote.tukio hilo lilionakana wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyo pembezoni mwa Mji( Peri Urban) katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Julai 11,2020.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja (katikati), akitoa maagizo kwa ujumbe alioambatana nao wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya Mradi wa kusambaza Umeme katika Vijiji vilivyopo pembezoni mwa Mji (Peri Urban) alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Julai 11, 2020.
************************************
Na Zuena Msuya, Pwani 0714 214950
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja ameionyooshea kidole Kampuni ya ukandarasi ya Namis inayotekeleza mradi wa kusambaza umeme katika Vijijini vilivyopo pembezoni mwa Mji (Peri Urban) Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, na Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam kwa kusuasua kutekeleza mradi huo na kuiagiza kuongeza kasi hadi kufikia mwishoni mwa Agosti, 2020 iwe imekamilisha kazi ya utekelezaji wa mradi huo.
Mhandisi Masanja alisema hayo, Julai 11, 2020 wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa kwa kasi isiyoridhisha, ikilinganishwa na makubaliano na matakwa ya mkataba husika, huku mkandarasi akieleza sababu zisizokubalika zinazochangia kusuasua kwa mradi huo.
Mhandisi Masanja alieleza kuwa, kwa sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 39 ambayo ni tathmini ya chini na makubiliano ya mkataba yanayoelekeza kuwa tangu kusainia kwa mkataba huo na kuanza kwa utekelezaji wa mradi mwezi Desemba, 2019, hadi kufikia sasa mradi huo ulitakiwa kuwa umekamilika kwa 77%.
Aidha alimtaka mkandarasi huyo kuongeza nguvu kazi na magenge ya watu watakaofanya kazi usiku na mchana ili kwenda sambasamba kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike ndani ya muda uliopangwa.
Vilevile alimshauri mkandarasi huyo kununua vifaa vya kutekeleza mradi kama nguzo, vyaya, LUKU, na vifaa vingine vinavyohitajika katika ujenzi wa mradi huo kutoka kwa wazalishaji wenye uwezo wa kuzalisha vifaa hivyo ili kurahisisha na kukamilisha hataka utekelezaji wa mradi huo.
“Hii kasi hairidhishi kabisa, utekelezaji wa mradi unasuasua, hizi sababu unazoeleza kuwa zimechangia kukuchelewesha wala zikubali kwa kuwa kuna wakandarasi wenzako mmeanza kazi pamoja na wote mmelipwa fedha sawa, cha kushangaza wenzako wamepiga hatua mbele na watamaliza kwa wakati, wewe ni nini kinakukwamisha, hakuna sababu za msingi katika hilo, kizuri zaidi vifaa vyote vinatengenezwa na kupatikana hapa nchini, kwakweli jipime na ujitafakari! hatutakubali!,”alisema Mhandisi Masanja.
Kwa mujibu wa Mhandisi Masanja, kampuni ya NAMIS ilipewa jukumu la kusambaza umeme katika vijiji 62 vya Peri Urban, kati ya hivyo vijiji 32 viko maeneo ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam na vijiji 30 viko maeneo ya Kisarawe, kazi ya utekelezaji wa mradi huo inaendelea lakini kwa kasi isiyoridhisha.
“Mkandarasi ameahidi na tumekubaliana kuwa hadi kufikia Julai 15, 2020 nguzo zote zilizosimikwa ziwe zimevutwa nyaya katika maeneo yote ya mradi, na kwamba ataendelea kuchimbia nguzo na kuvuta waya katika maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa, sambasamba na hilo ataunga wateja katika maeneo hayo, na mimi nitakuja tena mwishoni mwa mwezi huu kukagua kazi hii, na kila kitu kitajulikana hapo”.
Kampuni ya NAMIS ilipewa jukumu la kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miezi tisa ambapo mkataba wa utekelezaji ulianza Desemba 10, 2019 na utakoma Septemba 9, 2020 kwa kukamilisha kazi zote za kusambaza umeme na kuunga wateja katika vijiji vyote 62 vilivyopembezoni mwa miji ( Peri Urban) katika maeneo ya Kisarawe mkoani Pwani na Ilala mkoani Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mhandisi Thomas Uisso alimuahakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa atakamilisha kazi hiyo kwa wakati kwa mujibu wa mkataba licha ya kuwa nyuma ya muda, p-9kwa kuwa miundombinu na vifaa vyote vinavyohitajika eneo la mradi vipo, na watakachofanya ni kuongeza nguvu kazi ili kazi hiyo ifanyike usiku na mchana na kwa haraka.
Amewaomba wananchi waliopo katika maeneo yanayopitiwa na mradi huo kujiandaa kuunganishiwa umeme kwa kutandaza nyaya katika nyumba zao na kulipia gharama za kufungiwa umeme huo ambayo ni shilingi 27,000 tu.
Ikimbukwe kwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli aliyoifanya wilayani Kisarawe Mkoani Pwani,mwishoni mwa mwezi June mwaka huu 2020 aliiagiza Kampuni hiyo ya NAMIS kuvuta nyaya katika nguzo zote ilizozisimika katika wilaya hiyo.