***********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Rais wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) Bw.Paul Koyi pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwemo mabalozi wa Misri,Pakistan pamoja na Urusi wametembelea Maonesho ya Wafanyabiashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kupanua wigo wa biashara kati ya wafanyabiashara wetu na wa nje ya nchi.
Akizungumza baada ya kutembelea Maonesho hayo Bw.Koyi amesema kuwa wanajaribu kufanya juhudi hizo ili kuhakikisha wanatangaza biashara na kukuza biashara kwa wafanyabashara wetu waweze kufanya biashara na wenzao wa nchi za nje ili kuhakikisha uchumi wetu unaendelea kukua pamoja na ushirikiano wa kimataifa unakuwepo.
“Juzi tulikuwa na mkutano mkubwa na ubalozi wa Urusi kuhusu wafanyabiashara wa hapa na wa nchini Urusi na kuona fursa mbalimbali za biashara tunaweza kufanya hasa baada ya hili janga la Korona”. Amesema Bw.Koyi.
Aidha Bw.Koyi amesema mwezi Januari walikuwa na mkutano mkubwa na ubalozi wa Pakistani mjini kule Nairobi ambapo zaidi ya makapuni makubwa 200 yalikuja yakiwa yanazungumza biashara kati ya Afrika na Pakistani nao katika kufuatilia hilo wameendelea na mazungumzo nao bahati mbaya janga la Korona likaharibu lakini saizi wanarudi pamoja ili kuweza kuona wanaweza kufanya biashara hizo namna gani.
“Makampuni makubwa ya Misri yako hapa yanafanya kazi kwenye miradi mbalimbali haya ni matokeo ya juhudi kama hizi ambapo tunajaribu kuwaweka pamoja wafanyabiashara wetu waweze kufanya biashara na wafanyabiashara wa kule”.Amesema Bw.Koyi.
Pamoja na hayo Bw.Koyi amesema wapo katika juhudi za kutengeneza ujumbe wa pamoja ili kuweza kuratibu biashara kati ya Tanzania na Misri.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara (TANTRADE) Bw.Boniface Ngowi amesema kuwa wamehakikisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla ambao wanashiriki kwenye maonesho wanakuwa salama hasa katika janga hili la Korona.
“Kupitia pale getini watembeleaji hasa wale wanaonunua tiketi kunakuwa na utaratibu wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na wakiingi ndani kuna utaratibu ambao tumepewa na Wizara ya Afya kumpima kila mtu joto lake kama liko juu au liko chini, baada ya hapndani pia kuna maboresho mengi kwani kila banda tumeweka maji tiririka na sabuni”.Amesema Bw.Ngowi.
Aidha Bw.Ngowi amesema japo kuwepo kwa tishio la ugonjwa wa Korona wafanyabishara kutoka nje ya nchi wameshiriki kwa wingi ingawa nchi baadhi zilitakiwa kushiriki na hazikushiriki kutokana na kuwa lockdown.