…………………………………………………….
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Mwenyekiti wa Chama cha CUF Professa Ibrahim Lipumba ametoa wito kwa Chama cha Mapinduzi(CCM) na vyama vyote vya siasa nchini kufanya kampeni kwa kistaarabu na washindane kwa hoja ili kuwapa fursa wananchi kufanya chagu bora kwao katika Uchaguzi Mkuu ifikapo Oktoba 2020.
Wito ameitoa leo Jijini Dodoma wakati akitoa salamu wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa(NEC).
Aidha Profesa Lipumba amewatahadharisha CCM kuwa na CUF ipo inakuja katika uchaguzi wa Oktoba 2020 hivyo wajipange vyema.