…………………………………………………………………………………….
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, wamempitisha Dkt. John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kwa kura 1822 ambayo ndio idadi ya wajumbe waliohudhuria na ni asilimia 100 ya kura zote na hakuna kura zilizoharibika.
Aidha Dkt. Magufuli baada ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais CCM, pia amemteua Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza kwa awamu nyingine ya pili.
Dkt. Magufuli amesema kuwa hakutegemea kupigiwa kura na wanachama wa CCM na kupata kura asilimia mia.
“ Kura mlizonipigia zisinipe kiburi, zisinifanye nijione bora sana bali zikanipe nguvu za kuwatumikia Watanzania wote bila ya kuwabagua dini zao, Imani, dini, kabila zao”ameeleza Dkt. Magufuli
“Wajumbe wa mkutano mkuuu mmenipa heshima kubwa kwa kunipitisha kuwa mgombea wa Urais 2020 lakini na mimi nimebaki na ahadi kubwa kwenu na ninaomba Mungu kura nilizozipata leo zisinipe kiburi bali nguvu ya kuwatumikia Watanzania hasa wasiojiweza,”
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Zanzibar kuhacha mambo ya UPemba na Unguja wachukue Zanzibar moja kwa ajili ya maendeleo ya Wazanzibar watafanikiwa halafu pia ameongeza kuwa Mwinyi amemzidi umri hivyo atasikitika sana kama watamchagulia mtu ambaye amenizidi umri kila siku aseme shikamoo inachosha na inatia aibu kunichagulieni mtu ambaye na yeye atasikia raha.
“Wakati nimechaguliwa kupeperusha bendera 2015 nilikuwa na wagombea wenza wawili niwaambie ukweli, alikuwa ni Mwinyi na Mama Samia, lakini muelewe ukishindanishwa na Mama lazima utashindwa, nikamwambia Mwinyi tulia ngoja niende na Mama.”ameweka bayana Dkt. Magufuli
Lakini Dkt. Magufuli amemwelezea Dkt. Hussein Mwinyi kuwa ni tofauti Sana na watoto wengine wa wakubwa, hajabeba urais wa baba yake ni mtu mpole na mkarimu.
“Hussein Mwinyi ni mnyeyekevu sana na kama atachaguliwa mtayaona matokeo yake. Achaneni na Mambo ya upemba na unguja. Mtafanikiwa”- Mwenyekiti wa CCM Taifa” amesisitiza Dkt. Magufuli
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Dk. Bashiru Ally ametaja sababu tano zilizowashawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kumpendekeza Rais John Magufuli kuwania tena nafasi ya urais
Matokeo ya kura za kumpitisha Dkt. Magufuli kuwa mgombea urais wa CCM Jumla ya wajumbe walioshiriki kupiga kura ni 1822, Idadi ya wajumbe waliopiga kura ni 1822, hivyo Jumla ya kura za ndio ni 1822 huku Jumla ya kura za hapana zikiwa ni sifuri na Hakuna kura iliyoharibika.
Naye Mgombea Urais CCM Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi akisema kuwa akichaguliwa kuwa wa Zanzibar atatumia staili ya Magufuli katika kupambana na rushwa, uzembe na ubadhirifu hivyo ameawaahidi wananchi wa Zanzibar kusimamia hayo yote.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi akizungumza kwa niaba ya marais wastaafu amesema kuwa kuhakikisha wajumbe wote wa CCM wanawashawishi Watanzania wote wapate kumchagua Dkt. Magufuli .