……………………………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Serikali imesema kuwa vyama vyote vya ushirika vitakuwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serkali za Mitaa ili kuimarisha utendaji wake na kupeleka uchumi mbele kwa kutekeleza shughuli zake kwa ufasaha.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakuu wa mikoa juu Ushirika ili kwenda kusimamia ushirika katika mikoa yao.
Mhe. Jafo amesema kuwa Tume ya ushirika ikifanya kazi chini ya TAMISEMI itafanikiwa zaidi kwani kutakuwa na uangalizi wa karibu juu ya utendaji, uendeshwaji wa shughuli za ushirika katika mamlaka ya serikali za mitaa.
“Wakuu wa Mikoa mnapewa mamlaka yote ya kuweza kusimamia ushirika katika maeneo yenu ili kuweza kufikia malengo katika kupeleka mbele uchumi wa mwanamchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla”,ameeleza Mhe. Jafo.
Aidha Mhe. Jafo amesisitiza kuwa Wakuu wa Mikoa wasimamie jukumu la ushirika kufanya vizuri katika maeneo yao ili ushirika kwenda mbele zaid.
Mhe. Jafo ameelekeza kuwa wakuu wa mikoa wote nchini baada ya mafunzo hayo wanatakiwa kufahamu vyama vya ushirika katika mikoa yao, changamoto za vyama hivyo na kufahamu ufanisi wa vyama hivyo katika mikoa yao.
“Hivyo naimani kubwa kama mlivyo weza kuimba na kusimamia vituo vya afya pia na katika ushirika naimani baada ya mafunzo haya mtaweza kufanya usimamizi imara na kuleta matokeo mazuri katika ushirika nchini”ametoa wito Mhe. Jafo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema kuwa niwakata sasa wa kuwajibika kwa kuangalia maeneo ya utendaji katika ushirika ili kuhakikisha ushirika unakuwa imara na unawajibika zaidi sit u kwa wanaushirika ila serikali ambao ndio waliyotengeneza mfumo huu.
“Tunafanya hivyo kwa sababu ushirika sio chombo cha binafsi lakini pia sio chombo cha umma kwahiyo uko katikati lazima uwajibike pande zote mbili kwasababu umeusisha na kuunganisha umma kwa maana ya wanachama na wananchi wanaoshiriki katika ushirika”, amebainisha Shigella.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amesema kuwa watahakikisha kwamba ndani ya kipindi cha sasawanafanya kazi kubwa kwa kumulika kila sehemu ili kukagua vyama vya ushirika na kuleta tija kwa wakulima wote nchini.
Hapi ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya ushirika watakao pewa dhamana ya kuongoza kuhakikisha wanaongoza kwa kanuni na taratibu zilizopo katika vyama hivyo vya ushirika ili kuleta ufanisi mzuri katika ushirika kama alivyo agiza Mhe. Jafo.