Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya akizungumza wakati wa uwekaji wa saini juu ya Mradi wa ujenzi wa maabara ya taifa ya mazao ya kilimo inayojengwa Jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki waliohudhuria hotuba ya Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya akizungumza wakati wa uwekaji wa saini juu ya Mradi wa ujenzi wa maabara ya taifa ya mazao ya kilimo inayojengwa Jijini Dodoma
Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa na Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya Mazao ya Kilimo, Albert Mwambafu wakati wa kutiliana saini ya Mradi wa ujenzi wa maabara ya taifa ya mazao ya kilimo inayojengwa Jijini Dodoma
Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa na Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya Mazao ya Kilimo, Albert Mwambafu wakionyesha Mkataba mara baada ya kusaini Mradi wa ujenzi wa maabara ya taifa ya mazao ya kilimo inayojengwa Jijini Dodoma
Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa na Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya Mazao ya Kilimo, Albert Mwambafu wakibadilishana Mkataba mara baada ya kusaini Mradi wa ujenzi wa maabara ya taifa ya mazao ya kilimo inayojengwa Jijini Dodoma
………………………………………………………………….
Na. Alex Sonna, Dodoma
Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya amemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya kuchunguza mazao kutekeleza mradi huo kwa ubora unao takiwa na kukamilisha kwa muda uliyopangwa.
Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma wakati wa uwekaji wa saini juu ya mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa maabara ya taifa ya mazao ya kilimo inayojengwa Jijini Dodoma.
Aidha Kusaya amesema kuwa serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza mradi huo hivyo ni lazima wao kama watendaji kwa kushirikiana na mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati na ubora unaohitajika ili kutumika kwa shughuli zake.
“Natoa wito kwa Mkandarasi kutumia muda wake vizuri ili kukamisha mradi huu kwa wakati uliyopangwa katika mkataba tuliyosaiini leo kwani pesa ya kutekeleza mradi ipo yote imekamilika hivyo sitegemei kusikia kikwazo chochote juu ya pesa”, ameeleza Kusaya.
Hata hivyo Kusaya ameongeza kuwa mkandarasi huyo akitekeleza mradi huo kwa ukamilifu , ubora unaohitajika na muda sahihi ni sehemu moja wapo ya yeye kujihakikishia kuendelea kupewa miradi mingine katika wizara ya kilimo kwnia miradi ipo mingi.
Naye Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taifa ya Mazao ya Kilimo, Albert Mwambafu amesema kuwa kwa mkataba waliyo Saini na serikali watahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa haraka sana kwani tayali wako nyuma ya muda hivyo watajitahidi kuhakikisha wanaendana na muda uliyopangwa ili kukamilisha mradi huo.
“Mradi huu utakuwa wa kipekee ili kuweka alama na kuhakikisha tunaonyesha uzalendo kwa kutekeleza mradi huu katika ubora unaohitajika na kamilisha kwa muda uliopangwa kwa ajili ya manufaha ya watanzania na vizazi vya watanzania vijavyo ili mradi huo kutekeleza majukumu yake yanayotakiwa”, amebainisha Mwambafu.