AKATAA KUHUSISHWA NA ASKOFU GWAJIMA
KADA wa Chama cha Mapinduzi ADVOCATE Methusela Gwajima, ametia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kawe, duru za habari zimeripoti.
ADVOCATE Gwajima amesema ametia nia kuomba ridhaa ya Chama kugombea na kusema akipata nafasi hiyo atalikomboa Jimbo la Kawe ambalo limekuwa chini ya upinzani kwa muongo mmoja, huku akisema wananchi wa Kawe wamekosa mambo mengi ya manufaa kwenye jimbo hilo ambalo lina watu wengi wasomi, wafanya biashara na wananchi wa kawaida kwa sababu ya kukosa mtu wa kuwaunganisha jambo ambalo limeleta ugumu katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
“Nikweli nimetia nia kupitia chama changu CCM na nimejipanga vizuri sijakurupuka na uwezo ninao kama unavyofahamu kazi ya Wakili (ADVOCATE) ni utetezi hivyo, nitawatetea wana Kawe. Chama kikinipa ridhaa nina imani nitaikomboa Kawe” Alisema
ADVOCATE Gwajima anafahamika kuwa ni Kada mwenye msimamo thabiti usioyumba na mara nyingi amekuwa akijitokeza waziwazi kutetea Chama cha Mapinduzi pale wanapotokea wapotoshaji na wapinzani wa maendeleo katika Serikali ya Awamu ya Tano.
Hata hivyo. alipopigiwa simu kufafanua kuhusu uhusiano wake na Askofu Josephat Gwajima na utata wa kunukuliwa na vyombo vya habari akisema hatogombea ubunge wala urais, alisema yeye hajawahi kutoa kauli hiyo na kwamba hata yeye ameona clip ikizunguka mitandaoni ikisema hayo maneno ambayo amesema siyo yake.
“Mimi ni ADVOCATE, siyo Mchungaji wala Askofu, labda tu niseme kwamba Askofu Josephat Gwajima ni ndugu yangu na kwa nafasi yake ya utumishi anayo haki ya kusema hayo wala siwezi kuingilia maamuzi yake ya kusema kuwa na yeye anagombea Kawe kupitia CCM. Hivyo, tukiachie Chama cha Mapinduzi wao ndiyo wanafahamu mwanachama halali na nani anayefaa” Alisema Advocate Gwajima.