…………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Jumla ya wananchi elfu 15 kutoka vijiji vya Mandera, Magole A na B Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamenufaika na mradi wa maji unaotekelezwa na Shirika la Winrock International chini ya mradi maji wa WARIDI.
Hayo yamebainishwa na Mhandisi kutoka Shirika la Winrock International Zeidia John wakati akitoa taarifa ya mradi wa maji uliotekelezwa na Shirika hilo Wilayani Kilosa.
Zeidia ameongeza kuwa Shirika hilo inashirikiana na Serikali inatekeleza mradi wa WARIDI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani ambapo umeshanufaisha wananchi wilayani humo.
Akizungumza katika Kijiji cha Mandera Mtendaji wa Kijiji hicho Gladness Ntabwene amesema kuwa kabla ya mradi huo kuwepo jumla ya wananchi 5293 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 walikuwa wanapata maji kijiji hapo.
Ameeleza kuwa mpaka sasa jumla ya wananchi 6300 wamenufaikia na mradi huo katika kijiji chake na kusaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa maji kwa asilimia 80.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs iliyo chimi ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Timothy Mgonja amelipongeza Shirika la Winrock International kwa kusaidiana na Serikali kutatua changamoto katika jamii hasa changamoto za maji katika maeneo mbalimbali.
“Niwapongeze Shirika na wananchi kwa pamoja kwa kutekeleza mradi huu hakika tumeuona na tumejionea kwa macho kilichofanyika” alisema
Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Mandera Gladness Ntabwene amesema jumla ya wananchi 6300 wamaenuaika na mradi wa maji safi na salama uliotekelezwa na Shirika la Winrock International kwaufadhili wa watu wa Marekani.
Mmoja wa mnufaika wa Mradi huoSikuzani Shaban amushukuru Uongozi wa kijiji, Wilaya na mkoa kwa kuwaruhusu wafadhili hao kuleta mradi kijiji hapo na kutatua changamoto za upatikanaji wa maji.
Naye mjumbe wa Kamati ya Maji ya Kijiji hicho Hamza Saleh amesema kuwa wananchi wameshiriki kwa ukaribu katika kuchimba mitalo na kufukia mabomba ya maji hivyo kuufanya mradi kuwa na wananchi katika kuulinda ili hudumu kwa muda mrefu.