Home Mchanganyiko TAKUKURU YAIMARISHA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA SHULE ZA SEKONDARI

TAKUKURU YAIMARISHA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA SHULE ZA SEKONDARI

0

……………………………………………………………………………………………………..

Na John Walter-Babati

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara,  imeendelea kutoa elimu katika makundi mbalimbali ya jamii ili kuhakikisha adui rushwa anatokomea nchini.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu leo Julai 9,2020 amewatembelea wanafunzi katika shule ya Sekondari Bagara iliopo mjini Babati  ambapo aliwataka  wanafunzi hao kuzidisha  mapambano dhidi ya rushwa kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wenzao.

Hata hivyo Takukuru mkoani hapa kupitia kwa mkuu wa dawati la Elimu kwa Umma Sultan Ng’aladizi, imekuwa ikitoa elimu  kwa njia ya semina  midahalo, Mikutano ya Hadhara na kwenye vyombo vya habari.

Makungu amewasisitiza wanafunzi  hao kusoma kwa bidii na kuwaachia  neno la Mungu  kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia,  Mithali 22:5 unaosema  “Mlee mtoto katika njia impasayo,naye hataiacha,hata atakapokuwa mzee”.