……………………………………………………………………………………………………..
Na John Walter-Babati
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara, imeendelea kutoa elimu katika makundi mbalimbali ya jamii ili kuhakikisha adui rushwa anatokomea nchini.
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu leo Julai 9,2020 amewatembelea wanafunzi katika shule ya Sekondari Bagara iliopo mjini Babati ambapo aliwataka wanafunzi hao kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wenzao.
Hata hivyo Takukuru mkoani hapa kupitia kwa mkuu wa dawati la Elimu kwa Umma Sultan Ng’aladizi, imekuwa ikitoa elimu kwa njia ya semina midahalo, Mikutano ya Hadhara na kwenye vyombo vya habari.
Makungu amewasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwaachia neno la Mungu kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia, Mithali 22:5 unaosema “Mlee mtoto katika njia impasayo,naye hataiacha,hata atakapokuwa mzee”.