Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) Bw. Tumaini Nyamhokya,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa wawakilishi wa vijana wa TALGWU Taifa yanayofanyika jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) Bw. Tumaini Nyamhokya,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili kwa wawakilishi wa vijana wa TALGWU Taifa yanayofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) Tumaini Nyamhokya amewataka vijana wa chama hicho kuyatangaza mafanikio ya chama yaliyokwishapatikana ili kujenga Taswira njema kwa wanachama walio ndani hata kwa wale wasio wanachama wa (TALGWU).
Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Bw. Nyamhokya wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa wawakilishi wa vijana wa TALGWU Taifa ambapo amesema vijana hao hawana budi kuwa mstari wa mbele kusambaza taarifa njema na kuachana na baadhi ya mitandao ambayo imekuwa na dhamira isiyo njema ya kuharibu chama kwa kusababisha migogoro na migongano isiyo na lazima.
“Achaneni na haya magazeti yanayoandika habari potofu na mnajua kwanini yanaandika ,maana tayari yanachukuliwa hatua ,Mwenyekiti na Katibu mkuu tayari wanayashughulikia ,muwe mnajiongeza kwa hivyo niseme muwe wasemaji wazuri na muyafikishe haya tunayoyafanya hata nje ya chama.”ameeleza
Amesema awali walipoingia madarakani hawakuwa na umoja na hali hiyo ilisababisha kukwama kwa mambo mengi nda ni ya chama hicho lakini sasa kutpkana na ushirikiano na mshikamano uliopo umewawezesha kujenga taswira njema na hivyo kuwawezesha kushughulikia changamoto mbalimbali ndani ya chama ikiwemo suala la vyeti feki kwa wanachama.
“Mtihani namba moja ulikuwa niwa vyeti feki nah ii ilikuwa ni ngumu mimi kama mwenyekiti wa ile kamati ,lakini tulipigana kufa na kupona na hawa wazee tukaja Dodolma Zaidi ya mara nane yaani ni vikao hadi wakati mwingine tunagombana ,Tunakuja na TALGWU huku tunasimamia kofia ya (TUCTA) sababu TALGWU ndo tumeathirika Zaidi .”Ameongeza
Kwa upande wake Katibu mkuu wa TALGWU Taifa Rashid Mtima amesema wao kama viongozi wakuu wa chama wameona haja ya muda mrefu ambayo kuna mazingira yaliyowakwamisha kutofanya vikao vya pamoja na hivyo vijana waliopata nafasi ya kuwawakilisha vijana wenzao ni lazima watambue kuwa wanao wajibu wao na watambue nini chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa,wajue majukumu yao na wajibu wao kutoka katika maeneo wanayotoka.
“Nyinyi Vijana ndio mfano mzuri kabisa wa kubadilisha fikra na mitizamo ya vijana kutopenda vyama vya wafanyakazi kuliko hao wengine ,kwa hiyo haja ya nyinyi kukutana kuwanoa ,kuwapa misingi ya vyama vya wafanyakazi ,kuwaambia uwepo wa vyama vya wafanyakazi sio bahati.”Amesema
Naye Mwakilishi wa vijana wa TALGWU Taifa Ibrahim Swalehe amesema yapo mambo toka kuanzishwa kwa chama hicho yamefanywa ikiwemo[H1] muundo wa uajiri ambapo chama kiliona ni vyema kikaajiri watumishi wa TALGWU wanaotokana na serikali za mitaa ikiwa ni moja ya badiliko kubwa ambalo limekuwa shirikishi kwa jamii wanayoihudumia.
“Hili lilitoa fursa kwa waajiri wa serikali za mitaa ,tuwe waajiriwa wa chama na tuwatete wanachama wenzetu ,leo makatibu wetu wa mikoa wasipofanya vizuri kuna wakati huwa wanasutwakutokana na kutowajibika katika nafsi zao.”Amesisitiza.