MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy,akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Mwenyekiti wa Chemba ya wafanya Biashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Deus Nyabiri,akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Bw.Haruna Kifimbo,akitoa kero za wafabyabiashara kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (SAC) Gilles Muroto,akizungumzia usalama unaofanywa na Jeshi la Polisi katika kuwalinda wafanyabiashara kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa wiki tatu hadi Juni 26, mwaka huu kwa taasisi mbalimbali mkoani humo zilizolalamikiwa na wafanyabishara kwa utendaji mbovu kuandaa majibu ya kero hizo.
Agizo hilo imetolewa leo wakati wa Mkutano wa wafanya biashara na uongozi wa mkoa wa Dodoma uliyofanyika mkoani humo.
Dk Mahenge amesema kila taasisi itapelekewa orodha ya kero walizolalamikia wafanyabiashara na itatakiwa kuyafanyia kazi na kueleza utatuzi wa kero hizo katika mkutano wa marejeo Juni 26, mwaka huu.
Baadhiya taasisi zilizolalamikiwa ni pamoja na Jiji la Dodoma hasa wa Mipango Miji wamelalamikiwa kwa urasimu na ucheleweshaji vibali na utendaji usioridhisha.
Pia walilalamikia Kituo cha Mabasi kutowapanga utaratibu mzuri na kusababisha kutofanya vizuri kutokana na kutokuanza kwa baadhi ya huduma katika kituo hicho cha mabasi.
Wafanyabiashara hao walilalamikia utaratibu ulitumika kupanga wafanyabiashara katika Soko la Ndugai ambapo hawakushirikishwa wafanyabiasharana kupangisha kwa bei kubwa kutozwa sh 15,000 kila mita ya mraba na upangaji uliwasahau wajasiriamali wadogo.
Lakini pia wafanyabiashara kulazimishwa kwenda kutoa ushuru mkubwa katika soko la Ndugai na kutakiwa kupeleka bidhaa zao kuuza katika masoko wanayofanyia biashara kitendo kinachosababisha hasara katika biashara zao.
Kwa kuendelea wafanyabiashara walilalamikia uchafu wa masoko hasa la Majengo la Sabasaba kwamba uchafu umekithiri katika maeneo mbalimbali ya masoko hayo.
Wafanya biashara hao walieleza kuwa kampuni ya Usafi wa Mazingira kutokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kuzoa taka katika maeneo mbalimbali na sasa jiji kuwa chafu kutokana na kushindwa kufanya kazi hiyo.
Pia walilalamikia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) kutokana na kushindwa kutoa vizuri huduma za maji wakasema kwamba inaongekana kuna mgao lakini hawajaambiwa kama upo.
Aidha walilalamikia Sumatra kwamba inatesa wananchi kwa kuweka vituo vya kushuka au kupanda mbali kutoka kati ya mji, mfano mtu anayeenda Arusha asipopanda NaneNane anatakiwa kwenda Veyula umbali wa takaribani kilometa 20 ndipo akapande.
Mwenyekiti wa Chemba ya wafanya Biashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Deus Nyabiri amesema viongozi wa serikali wanatakiwa kushirikiana na wafanyabiashara katika kuhamasisha uwekezaji katika jiji hilo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Mafuta Dodoma, Faustine Mwakalinga amesema watendaji wa Jiji wamekuwa wakiendeleza urasimu na vitendo vya rushwa wamekuwa wakiweka alama za X na mtu akitoa chochote wanafuta alama hiyo ndani ya muda mfupi.
Naye Mkurugenzi wa Duka na Nguo (Peter Fashion) Peter Ulomi ameeleza tatizo la maji ni kubwa, hawajui kama kuna mgao au namna gani kwani wamekuwa wakikosa maji na hawapewi taarifa yoyote kama kuna mgao ili kujipanga.
Huku Haruna Kifimbo amebainisha kuwa katika soko la Ndugai wadau hawakushirikishwa na waliopewa maeneo si wafanyabiashara bali watumishi wa ofisini.
Kifimbo ametoa wito kwa Mkuu wa Mkoa aitishe mkutano wa wafanyabiashara wa masoko yote katika jiji hilo ili kutafuta suluhisho la masuala ya usafi na changamoto nyingine zinazowakabili.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy ameelekeza wafanyabiashara kujipanga kwa kuboresha mazingira ya kufanyia biashara kwa kuacha kupanga bidhaa chini na waache kungoja serikali kuwaelekeza suala hilo.