Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi 21 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) kwa mwaka 2020 hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi 21 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) kwa mwaka 2020 hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Meneja wa Kanda ya Kati CRDB Benki, Chabu Mishwaro akitoa akieleza mchango wa CRDB katika kufanyikisha zawadi kwa washindi 21 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) kwa mwaka 2020 hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Kati VODACOM, Grace Chambua akitoa neno wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi 21 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) kwa mwaka 2020 hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikabidhi zawadi kwa baadhi ya washindi 21 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) kwa mwaka 2020 hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na washindi mara baada ya kuwakabidhi zawadi washindi 21 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) kwa mwaka 2020 hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
…………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 870 ili kuwaendeleza wabunifu na bunifu zao kwa Maendeleo ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi 21 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojiana Ubunifu (Makisatu) kwa mwaka 2020 iliyofanyika jijini Dodoma.
Aidha washindi wa mashindano ya kitaifa ya Sayansi na Teknolojia na ubunifu MAKISATU wametunukiwa vyetu na zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kila kundi amezawadiwa milioni tano, wa pili milioni tatu na wa tatu milioni mbili.
Nasha amesema kuwa mashindano hayo yanaumuhimu mkubwa hasa katika wakati huu nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo Teknolojia na ubunifu wa ndani ni muhimu Sana ili nchi iendelee kuimarika na kukua zaidi.
” Kama mnavyojua wakati sisi tunapanda kutoka uchumi wa chini kwenda juu, maana yake kuna nchi zilishuka hivyo na sisi Kama hatutawekeza kikamilifu hasa katika teknolojia itakuwa ni vigumu kudumu katika uchumi wa Kati” amesema Nasha.
Nasha ameongeza kuwa Serikali inathamini sana shughuri za ubunifu na itaendelea kuunga mkono kuhakikisha ubunifu wa Sayansi unakuwa hapa nchini na kuleta tija kwa jamii.
Nasha amesisitiza kuwa ni muhimu kuendeleza bunifu za kiteknolojia kwa sababu baada ya kuingia uchumi wa kati Sasa ushindani utakuwa mkubwa Sana tofauti na tulivyokuwa katika uchumi wa chini kwani hakukuwa na ushindani mkubwa wa teknolojia.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe, amesema mashindano hayo ya MAKISATU ni mkakati wa serikali kuibua na kuendeleza bunifu za kiteknolojia hapa nchini.
Prof. Mdoe amesema kuwa mashindano hayo yalianza mwaka 2019 na katika mashindano hayo yaliibua wabunifu sitini (60) na wote wapo katika hatua mbalimbali za kuendelezwa katika bunifu zao.
Prof. Mdoe ameeleza kuwa mashindano ya mwaka huu washiriki walioingia fainali walikuwa sabini(70) na wabunifu ishirini na moja (21) walipatikana ikiwa ni watatu kwa kila kundi huku akibainisha kuwa wabunifu wote sabini watapatiwa vyeti vya kuwatambua.
Kwa upande wake mmoja wa washindi wa shindano hilo Cecilia China kutoka kundi la vyuo vikuu ameishukuru serikali kwa kutambua ubunifu wao kwani kwani utawafanya wafanye kazi kwa bidii.
Makundi yaliyoshiriki katika shindano hilo ni Kundi la shule za msingi, shule za Sekondari, vyuo vya ufundi stadi, Vyuo vya Kati, taasisi za utafiti na maendeleo, vyuo vikuu na wabunifu kutoka kwenye mfumo usio rasmi.
Kauli mbiu ya mashindano hayo kwa mwaka 2020 ni ” Sayansi teknolojia na ubunifu kwa uchimi wa Viwanda”.