NA MWANDISHI WETU, SABASABA
MKURUGENZI Mwendeshaji wa FUKO wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bi. Sabra Issa Machano amefurahishwa na namna mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na ule wa NSSF kutumia banda moja katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaa wakati alipotembelea banda hilo Julai 7, 2020.
“Nimefurahi sana kufika hapa leo katika banda la pamoja la PSSSF na NSSF tayari Mfuko wetu
unaushirikiano na NSSF tutaangalia namna tunavyoweza kushirikiana na PSSSF ili
tuweze kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyakazi wanaohama kutoka Tanzania
Bara kwenda Zanzibar au Zanzibar kuja Bara.” A;lisema Bi. Sabra.

“Kuhama kwa wafanyakazi kutoka sehemu moja ya Tanzania iwe bara au Zanzibar kumepelekea changamoto ya kuwahudumia wafanyaakzi hao hususan katika suala la michango katika mifuko mitatu ya hifadhi ya Jamii yaani ZSSF ya Zanzibar kwa upande
mmoja na PSSSF na NSSF kwa upande wa Tanzania bara.” Alisema Mkurugenzi huyo na
kuongeza…..Changamoto kubwa inayoikabili mifuko hii mitatu kwa sasa ni movement ya wafanyakazi Tanzania ……. Na kwa
sasa hivi changamoto hii tumeiona hasa kwenye mahoteli, wafanyakazi wengi wa
mahotelini wanatoka Tanzania bara wanakuwa wanatamani kuhama wakati umefika
sasa tuangalie kwa wale wafanyakazi wanaofanya kazi Zanzibar na wanatoka
Tanzania bara au wale wanaofanya kazi Tanzania bara na wanatoka Zanzibar
wakihamia sehemu moja ya Tanzania tutawahudumia vipi, swala hili ni muhimu
tukaliangalia ili tulipatie ufumbuzi.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Bi. Sabra Issa (wapili kulia), akipokea mfuko wenye vipeperushi kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul Njaidi wakati Bi Sabra alipotembelea banda la ushirikiano la Mifuko ya PSSSF na NSSF kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 7, 2020. Wengine kushoto ni Meneja Mkuu, Uhusiano na Elimu kwa Umma, NSSF, Bi. Lulu Mengele na kushoto ni Bw. Juma Mmanga.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Bi. Sabra Issa (katikati) akizungumza na Afisa Uhusiano Mkuu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Abdul Njaidi (kushoto) na Meneja Mkuu, Uhusiano na Elimu kwa Umma, NSSF, Bi. Lulu Mengele wakati alipowasili kwenye banda hilo la ushirikiano.