…………………………………………………………………..
Na Jusline Marco-Arusha
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM Taifa Kheri James amesema kuwa asilimia 70 ya viongozi wanaoendesha vyama vya upinzani nchini ni matunda ya ccm hivyo amewataka wananchi kuondokana na mtazamo hasi kuwa kila mwanasiasa anayejiunga na chama hicho amenunuliwa.
Akizungumza katika mkutano maalumu wa kuwapokea wanachama wapya kutoka katika vyama vya upinzani akiwamo aliyekuwa mbunge ya Arumeru mashariki Joshua Nasaari na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Karatu Willy Qambalo(Kwambalo),mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ccm Mkoa wa Arusha.
Kheri amesema kuwa kumekuwa ni tabia kwa wapinzi kuwa mtu akihamia CCM amenunuliwa lakini mwanachama wao akihamia upinzani imekuwa ni demokrasia jambo ambalo huchukuliwa kawaida kwa chama cha mapinduzi kuwa kila mtu anayo haki ya kuhamia chama chochote.
“CCM hatuna nongwa kwa mtu atakayeacha imani ya chama cha mapinduzi na kwenda kingine kwani ni haki yake kufanya hivyo kwani chama chetu kimejipanga na kiko tayari kumkabili kiongozi yeyote wa upinzani,”alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema wao kama vijana wako karibu na Rais John Magufuli kutokana na ameleta maendeleo nchini katika sekta mbalimbali kitu na kuondoa ubinafsi jambo ambalo lilikuwa la kawaida katima uongozi uliopita.
Hata hivyo aliyekuwa mbunge wa jimbo laArumeru Mashariki,Joshua Nasari alisema sababu za kuhama chama cha demokrasia na maendeleo
(Chadema) ni Rais Magufuli kuondoa changamoto za wananchi wa jimbo hilo kama migogoro ya ardhi.
“Kitu alichokifanya Rais huyu kilinifnya nitafakari sababu za kutompinga kwani nilikuwa najitahidi kuleta maendeleo katika jimbo langu lakini nilikumbana na vikwazo kwa baadhi ya viongozi lakuni Magufuli aliruhusu,”alisema Nasari .
Nasari alisema kwamba kuhamia kwake CCM siyo kwa nia ya kutakangaza nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi bali amehania ili kuunga mkono na kuendeleza juhudi za Rais Magufuli alizofanya ndani ya miaka mitano kwa wananchi wa Arumeru kupitia chama hicho.