Home Mchanganyiko WAZIRI JAFO ATAKA DAMPO LA KISASA JIJINI TANGA LILINDWE

WAZIRI JAFO ATAKA DAMPO LA KISASA JIJINI TANGA LILINDWE

0

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo akizungumza na watumishi
wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua miradi
mbalimbali ya kimaendeleo Jijini Tanga

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo akizungumza mara baada ya kukagua miradi mbalimbali
ya kimaendeleo wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo kushoto akizindua Jengo la
Halmashauri ya Jiji la Tanga leo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
Thobias Mwilapwa

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo kushoto akiwa na
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga mara baada ya kutembela ujenzi wa Jengo la
kitega uchumi cha Stendi ya Mabasi Jijini Tanga kushoto ni Katibu Tawala
wa wilaya ya Tanga Faidha Salim

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo katikati akitoka kwenye
Jengo la Halmashauri ya Jiji la Tanga mara baada ya kulikagua kushoto ni
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na kulia ni Katibu wa CCM
wilaya ya TangaWAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo wa pili kutoka kushoto
akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati
alipotembelea mradi wa  kitega uchumi cha stendi ya mabasi kange Jijini
Tanga wakati wa ziara yake wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
Thobias Mwilapwa

Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo

Ujenzi
wa Jengo la Kitega Uchumi cha Halmashauri ya Jiji la Tanga kwenye
stendi ya Mabasi Kange Jijini Tanga mafundi wakiendelea na ujenzi

Muonekano wa Jengo jipya la Halmashauri ya Jiji la  Tanga

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo ametaka dampo la kisasa la Mpirani Jijini Tanga lilindwe kwa sababu ni uchumi na limetumia kiasi cha Bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wake mpaka lilipokamilika huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kwenda na viroba kuchukua kokoto.

Amesema kwani kokote hizo zimemwagwa kwenye dampo hilo kwa ajili ya kulinda dampo hilo ambalo litakuwa la kisasa kwa Jiji hilo tokea lilipoanzishwa huku akieleza ujenzi huo umetokana na mapenzi mwema ya serikali ya awamu ya tano Dkt John Magufuli kuwadumia watanzania.

Jafo aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake Jijini Tanga ambapo alitembelea mradi mbalimbali na kufanya uzinduzi ambayo ni ujenzi wa dampo la kisasa mpirani, ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Jiji hilo,Ujenzi wa mradi wa mkakati wa Jengo la kitega uchumi stendi ya mabasi .

Baada ya kutembelea dampo hilo alionekana kuridhishwa na ujenzi wake huku akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na watendaji wake ikiwemo wasimamizi wa mradi huo kutoka Tarura Makao Makuu.

Sambamba na maeneo hayo lakini pia Waziri huyo alitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Kange stendi kuu ya mabasi ambapo kote alipopita alionekana kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema katika maeneo mengine ya dampo wakati unapokwenda kutembelea unaona hofu ya kufika lakini kwenye dampo hilo tokea amefika hapo hakusikia harufu yoyote hivyo mkurugenzi na watendaji wake wamefanya kazi kubwa sana .

Waziri huyo alisema mradi huo umepata umafanikio makubwa kwani Tanga ya mwaka 2015 sio ya mwaka 2020 hivyo dada zangu walikuwa na viatu vya mchuchumio na nywele wanaweza kutengeneza vizuri lakini wanashindwa kutembea lakini kwa sasa wanaweza kutembela bila kuwepo na hofu.

“Pongezi kwa Jiji la Tanga ujenzi wa hospitali ya wilaya eneo la Masiwani mmepewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya leo nimepata taarifa huduma zinatolewa na Rais ametoa fedha nyengine za ujenzi wa vituo vyengine hapa Tanga maana yake wananchi waliokuwa wanatembela umbali mrefu sasa watapata huduma karibu tena vituo vilivyoboreshwea kwa kisasa”Alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo alisema kwamba watumishi wa halmashauri wasingesimama pamoja kwa ajili ya miundombinu hiyo ambayo imejengwa kwa gharama ya milioni 400 mpaka milioni 500 wakati vituo hivyo kwani kipindi cha nyuma vilikuwa vinajengwa kwa wastani wa bilioni 2 wakaelekeza vituo hivyo vijengwa kupitia fedha ya ndani (Force Acount).