Home Biashara PROF.SHEMDOE AIPONGEZA BRELA

PROF.SHEMDOE AIPONGEZA BRELA

0

Katibu mkuu wa Viwanda na Biashara ni Prof.Riziki Shemdoe akizungumza na uongozi na wafanyakazi wa BRELA hivi karibuni katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es salaamMkurugenzi Mtendaji wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akizungumza katika kikao Cha Katibu mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara na wafanyakazi wa BRELA kilichofanyika hivi karibuni katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es salaam

Baadhi ya wakuu wa vitengo wakifuatilia mkutano huo Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika mkutano huo

Katibu mkuu wa Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe amepongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)kwa kazi na hatua waliyofikia 

Ameyasema hayo baada ya kutembelea katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es salaam

“Nina zaidi ya mwezi mzima sijasikia lalamiko hata moja hii imeonesha kwamba kuna transformation ya hali ya juu ambayo mnaifanya”. Amesema Prof.Shemdoe.

Aidha Prof.Shemdoe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa BRELA kufuatilia makampuni ambayo yapo mengi ambayo hayaeleweki hivyo kama kuna uwezekano yakafutwa.

“Nina taarifa yakuwa BRELA tunayo makampuni mengi ambayo ninayaita domant, watu wanamakampuni lakini hayapo mahali popote tunaita yameegeshwa, Mkurugenzi nikuombe liangalieni hili suala kama ni suala la kikanuni au kisheria tuandikieni ili bunge litakaporejea tuwe na kitu cha kupeleka”.Amesema Prof.Shemdoe.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu BRELA Bw.Godfrey Nyaisa ameelezea changamoto walizonazo zikiwemo ni pamoja na changamoto ya watumishi ambao wanaotoa maamuzi ambapo mpaka sasa BRELA ina watumishi wawili.

“Watumishi ni wachache wakati mwingine maombi yanakuwa ni mengi ambapo inawalazimu kufanya kazi muda ambao si wa kazi wakiwa majumbani kwao”. Amesema Bw/Nyaisa.