Home Biashara NCHI ZINAZOZUNGUKA ZIWA VICTORIA ZATAKIWA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI HUSIKA

NCHI ZINAZOZUNGUKA ZIWA VICTORIA ZATAKIWA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI HUSIKA

0

NAIBU  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza  katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa nchi zinazozunguka Ziwa Victoria uliofanyika kwa njia ya Video Conference (mtandao) ikiwa ni njia ya kuendelea kupambana na virusi vya Corona  ukihusisha  nchi za Kenya, Uganda, Burundi na Tanzania jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa  mkutano wa Baraza la Mawaziri wa nchi zinazozunguka Ziwa Victoria uliofanyika kwa njia ya Video Conference (mtandao) ikiwa ni njia ya kuendelea kupambana na virusi vya Corona  ukihusisha  nchi za Kenya, Uganda, Burundi na Tanzania jijini Dodoma.

 ………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna, Dodoma

NAIBU  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amezitaka nchi zinazozunguka Ziwa Victoria kuhakikisha zinalinda raslimali za nchi husika ikiwemo kupiga vita uvuvi haramu kwa manufaa ya taifa na raia wake .

 Wito huo umetolewa  katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa nchi zinazozunguka Ziwa Victoria uliofanyika kwa njia ya Video Conference (mtandao) ikiwa ni njia ya kuendelea kupambana na virusi vya Corona  ukihusisha  nchi za Kenya, Uganda, Burundi na Tanzania ambapo alisema ajenda hiyo ni endelevu.

Aidha Ulega amesema kuwa miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa ni pamoja na kuiwezesha Taasisi ya Lake Victoria Fisheries Organization inatekeleza majukumu yake katika hali ya ustawi kuendeleza sekta ya uvuvi  katika nchi hizo ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa na kutoa huduma ya chakula kwa wananchi.

“Sekta hii imekuwa na mchango mkubwa asilimia zaidi ya 60% ya mapato yanatoka katika Ziwa Victoria pia inawapatia watu ajira, chakula na hata biashara watanzania nao ni mashahidi nchi yetu inasafirisha minofu kutoka Mwanza kwenda nchi za Ulaya katika Ziwa Victoria hivyo hatuna budi kutumia raslimali hii vizuri”ameeleza Ulega.

Ulega amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo  ina eneo kubwa katika Ziwa hilo kuliko nchi zingine hali ambayo inatoa chachu kwa watanzania kutumia fursa hiyo kujiendeleza kiuchumi na kupambana na umaskini kundokana na maisha ya utegemezi.

Ulega ameeleza mchango wa wananchi katika sekta hiyo alieleza kwamba Tanzania ina wavuvi wasiopungua  200,000 ambayo wanajihusisha katika nyanja mbalimbali huku wananufaika na mnyororo  wa thamani wakifikia zaidi ya milioni nne ikiwa ni azma ya serikali ya awamu ya tano kutetea na kusimamia hali bora ya maisha kwa wananchi wake.

“Mchakato huu siyo kwamba utaishia kiazi hiki tu tunafanya kwa ajili ya kizazi kijacho cha watoto wetu sasa serikali haiwezi kufikia lengo hili peke yake bila kuunganisha nguvu na wananchi kwasababu sisi ndiyo walinzi wa kwanza lazima tuwe na uchungu na vyetu kama tunavyoona inatusaisia kuendesha maisha na kuinu auchumi wan chi yetu basi kila mmoja aone ana cha kufanya kufikia matamanio yetu” amesisitiza Ulega.

 Amehitimisha kwa kusema kuwa baada ya mkutano huo yanatarajiwa mabadiliko makubwa katika sekta ya Uvuvi kwa kila nchi kuona namna inavyoweza kufanya kuendelea kutoa elimu kwa raia wake kuhusu manufaa ya Uvuvi akieleza kwamba wanufaika wakubwa ni wananchi wenyewe  huku akiongeza kwmaba mkutano ujao unatarajiwa kufanyika nchini Kenya.