Home Teknolojia CHUO CHA UALIMU WA UFUNDI STADI VETA-MOROGORO WAANDAA TEKNOLOJIA RAHISI YA KUFUNDISHA...

CHUO CHA UALIMU WA UFUNDI STADI VETA-MOROGORO WAANDAA TEKNOLOJIA RAHISI YA KUFUNDISHA FANI YA UMEME VIWANDANI

0

**********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi VETA-Morogoro kimeweza kuandaa mfumo ambao utatumika kwaajili ya kufundishia kwa vitendo fani ya umeme wa viwandani ili kuweza kuwaandaa watendaji wa viwanda waliomakini.

Akizungumza katika Maonesho ya 44 ya biashara ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkufunzi Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi VETA-Morogoro Mhandisi Enelisa Andengulile amesema wameamua kuja na teknolojia rahisi wa kufundisha umeme wa viwandani kwa kutumia kompyuta (Electrical Simulater)

“Mwanafunzi anafundishwa kwenye kompyuta jinsi anaweza kufanya shughuli za kiwandani na baadae anaanza kujifunza kwa vitendo hivyo kulingana na kuwa ameshajifunza kwenye kompyuta anapokuja kwenye practical anaelewa kwa urahisi sana kuliko kufanya kwa kukisia”. Amesema Mhandisi Enelisa.

Aidha Mhandisi Enelisa amesema atuwezi kuzalisha ajira kama hatujawazalisha kwanza nguvu kazi na kuwafundisha kwanza kuwazalisha darasani hivyo tumekuja na teknolojia rahisi ya kuwafundisha kwa haraka na kwa uelewa mkubwa na kwenda kufanya kazi viwandani hivyo tutakuwa tumezalisha ajira pamoja na kuweza kufanikisha biashara za viwanda kuwa endelevu.