Mwalimu wa fani ya Mifugo Chuo cha Veta-Singida Bw.Ladslous Chemele akizungumza na baadhi ya wateja waliofika katika banda la VETA katika Maonesho ya 44 ya biashara ya Sabasaba katika Viwanja vya Walimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
***********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wafugaji wanaoanza kufuga wanyama au ndege wametakiwa kuonana kwanza na wataalamu kufahamu ni njia zipi wafuate ili kuweza kufanikiwa kufuga kwa ufasaha.
Akizungumza katika Maonesho ya 44 ya biashara ya Sabasaba katika Viwanja vya MWalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa fani ya Mifugo Chuo cha Veta-Singida Bw.Ladslous Chemele amesema wafugaji wengi wamekuwa wakikwama katika fani ya ufugaji kutokana na wengi wao wanaanza ufugaji pasipokuonana na wataalamu ambao wangempatia ushauri wa ziada namna ya ufugaji bora na wenye tija.
“Akija kwetu lazima tumuulize maswali anataka afuge nini na anauwezo kiasi gani pamoja na eneo ambalo anafugia anaweza akasema anataka kufuga kuku elfu 5 kumbe yeye anaeneo ambalo kwa kuku hao wengi halifai”. Amesema Bw.Chemele.
Aidha Bw.Chemele amesema wanatumia malighafi mbalimbali yanayopatikana hapahapa nchini kutengeneza vyakula vya mifugo hivyo lazima iwe na uwiano sahihi na muongozo ambao wanautumia kutengeneza hivyo vyakula.
“Wahitimu wanahajirika kwa kiasi kikubwa kwani wengi wamekuwa wakijiajiri na wengine kuajiriwa kwa haraka pindi wanapohitimu masomo ya fani ya mifugo”. Amesema Bw.Chemele.
Kujiunga na chuo hicho cha fani ufugaji Mkoa wa Singida unatakiwa kufika chuo chochote cha VETA kilichgo karibu kupata fomu kwaajili ya kujiunga na chuo hicho hivyo fomu zinapatikana kuanzia mwezi wa nane na vyuo kuanza mwezi Januari.