***************************
NA EMMANUEL MBATILO
Chuo cha Ufundi VETA Mkoa wa Singida kupitia kwa wanafunzi wake wametengeneza mfumo wa Umeme majumbani ambao utaweza kusaidia indapo giza likiingia taa hujiwasha yenyewe.
Akizungumza katika Maonesho ya 44 ya biashara katika viwanja vya Sabasaba vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mwanafunzi wa Chuo cha Sabasaba Mkoa wa Singida Bw.Masome Stephano amesema wameamua kutengeneza jifaa cha kuhisi giza na kuweza kuwasha umeme kuwasaidia watu ambao hawashindi nyumbani na kurudi usiku.
“Endapo ukiwa umeecha taa umezima hivyo giza likiiingia tu kama umefunga mfumo huu wa umeme taa hujiwasha zenyewe hivyo ni usalama kwako pindi ukiwa haupo, mtu mwenye nia mbaya kwako hatojua kama upo au haupo maana taa zitakuwa zimewashwa”. Amesema Bw.Masome.
Aidha kifaa hicho kitafanya kazi tu endapo taa zako zimezimika kwani kifaa hicho huwa kina hisi giza ndipo hujiwasha.