Mjumbe wa kikao hicho, Aisha Sinda ambaye ni Wakili wa Kujitegemea akizungumza jambo kwenye kiako hicho.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akiongoza kikao cha Baraza la Elimu ya Sheria la Tanzania Bara, kwa njia ya Mkutano Mtandao leo Jijini Dar es Salaam huku baadhi ya wajumbe wawili wakishiriki kwa mtandao nje ya jiji hilo. Jaji Kiongozi ambaye ni Mwenyekiti wa baraza hilo, ameongoza kikao hicho cha tathmini ya mchakato wa kupokea maombi , usahili wa kuwapokea na kuwakubali mawakili wapya uliofanyika hivi karibuni.
Mjumbe wa kikao hicho, Dkt. Erasmo Nyika ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School )akichangia hoja.
Katibu wa Baraza la Elimu ya Sheria la Tanzania Bara, ambaye pia Naibu Msajili Mkuu Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Messe Chaba, akitoa tathmini ya mchakato huo.