MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kulia akionyeshwa michoro mbalimbali ya kituo cha Polisi cha zamani wilayani Pangani na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi wakati alipokwenda kuwashukuru wasamaria wema wilayani humo waliojitolea ujenzi wa kituo cha Polisi ili kutokomeza uhalifu
Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Pangani wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kushoto akipata maelezo mapokezi wakati alipoingia kwenye kituo cha Polisi Pangani akiwa na kulia Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
kujitokea kufanikisha ujenzi wa kituo cha Polisi kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi
*************************************
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewapa mtihani mkubwa wakuu wa Polisi wa wilaya nchini (OCD) ambao watakutwa kwenye maeneo yao hawajafanya jambo lolote la kimaendeleo atalazimika kuondokana nao kutokana na kwamba watakuwa hawana tija.
IGP Siro aliyasema hayo wakati alipofika wilayani Pangani kwa lengo la kuwashukuru wasamaria wema waliojitolea kufanikisha ujenzi wa kituo cha Polisi wilayani humo juhudi ambazo zimefanywa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo Georgina Matagi.
Alisema kwamba kazi kubwa iliyofanywa na Mkuu huyo wa Polisi wilaya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inapaswa kuigwa na wakuu wengine hapa nchini huku akiwataka kuacha kuwa watu wa kulialia bali wahakikishe wanakuwa wabunifu kwa kuiga mfano wa OCD wa Pangani.
“MaOCD msiwe watu wa kulia muwe wabunifu kuiga mfano wa Mkuu wa Polisi Pangani (OCD) huku akimtaka kuendelea hivyo hivyo kwa sababu kwani kuna ma ocd mawe hawafikirii namna ya kusaidia jeshi anachojua ni kumsubiri IGP ampelekee fedha…IGP yupo sawa,Amri Jeshi Mkuu yupo,wewewni ODC na RPC kuna vitu unaaweza kujiongeza kwa kuwatumia wadau werevu kuweza kusaidia”Alisema IGP Siro.
“Lakini pia OCD umenipa changmoto mimi niko smati sana sijua imekuwaje nikaisahau Pangani mpaka wewe bwana mdogo ukaja kufanya hii kazi nzuri hongera sana kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha ujenzi huo unafanyika na kukamilika “Alisema
Aidha aliwashukuru wadau hao na OCD kwa kazi kubwa ya kulisaidia Jeshi la Polisi kujenga kituo hicho huku akiwaambie kwamba walichokifanya kwa faida ya watanzania wote kwa kuacha alama ya kesho na kesho kutwa haupo watu watakukumbuka hivyo kwa niaba ya Rais niwashukur sana kwa kazi nzuri mliyofanya kituo hiki huku nyuma hahakikuwa hivi msione mmepoteza bali mmeongeza fursa.
Hata hivyo alisema kwamba kuna vitu ambavyo havijakamilika hivyo nitatoa milioni tano huku akiwaomba wadau wa maendeleo nchi nzima walisaidie Jeshi la Polisi kwa sababu usalama ndio kila kitu wanakwenda msikitini na kanisani kwa sababu ya usalama na usipokuwepo ni hatari hivyo kila mtu ambaye mungu amemjalia kipato akiona mahali kuna shida ya kituo cha Polisi asaidie,kwani vituo hivyo vitawasaidia.
Akizungumzia suala la usalama IGP Siro alisema suala hilo ni muhimu sana na ukishavurujika ni vigumu sana kuweza kuurudisha huku akitolea mfano watu wa msumbuji kwa sabau usalama haupo hapa ni mpakani wakati wa uchaguzi watu wenye nia mbaya wanaweza kuleta mambo ya hivyohovyo watoe taarifa wasimuamini kila mtu ni vuzuri wakavijulisha vyombo vya ulinzi na usalama.
Alisema kwamba wakati wa uchaguzi lolote linaweza kufanyika wabaya wetu wakachukua nafasi kufanya mambo maovu wanaweza kuingia hivyo niwaombe mkiona ya namna hiyo hakikisheni mnatoa taarifa kwenye vyombo vinavyohusika ili kuweza kufanyiwa kazi mambo hayo.
Hata hivyo alisema usalama watanzania walioukuta wajitahidi sana kuulinda huku akisema wachache wanaotaka kuleta figisufigisu watahakikisha wanashughulikiwa na kurudishwa kwenye mstari.
Awali akizungumza Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Muheza alisema huo ni utekelezaji wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kupitia CCM kwamba lazima askari wawe na maeneo mazuri ya kufanyia kazi na wananchi waweze kupata huduma nzuri wadau hao wamejitolea kwa kushirikiana na serikali kazi kubwa imefanyika