Mch wa kanisa la EAGT Chamwino Ikulu ,Andrea Haule akitoa mahubiri kwa waumini wa Kanisa la EAGT Mlimwa jijini Dodoma kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Brown Mwakipesile katika adhimisho la Ibada Kuu.
Waumini wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) wakimsikiliza Mch wa kanisa la EAGT Chamwino Ikulu ,Andrea Haule wakati akitoa mahubiri katika adhimisho la Ibada Kuu leo jijini Dodoma.
Mch wa kanisa la EAGT Chamwino Ikulu ,Andrea Haule akisisitiza ujumbe kwa waumini wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) wakati akitoa neno la Mungu kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Askofu Brown Mwakipesile katika adhimisho la Ibada Kuu iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya waumini wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) wakifatilia Ibada Kuu kutoka kwa Mch wa kanisa la EAGT Chamwino Ikulu ,Andrea Haule wakati akitoa neno la Mungu kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Askofu Brown Mwakipesile katika adhimisho la Ibada Kuu iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Waumini wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) wakicheza nyimbo za kumuabudu Mungu wakati wa Ibada Kuu leo jijini Dodoma.
Kwaya mbalimbali zikiimba nyimbo za kumsifu Mungu katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) wakati wa adhimisho la Ibada Kuu iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mch wa kanisa la EAGT Chamwino Ikulu ,Andrea Haule akiwaombea baadhi ya waumini wenye matatizo mbalimbali wakati wa Ibada katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) wakati akitoa neno la Mungu kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Askofu Brown Mwakipesile katika adhimisho la Ibada Kuu iliyofanyika leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waumini wa Dini ya Kikristu wameaswa kumtegemea Roho Mtakatifu katiika kila jambo wanalolifanya katika Maisha yao ya kila siku ili waweze kupata mafanikio ya kimwili na kiroho ikiwa ni pamoja na kuitenda kazi ya Mungu katika roho na kweli na hivyo kuleta mabadiliko ya ndani.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma kwa niaba ya Askofu Mkuu wa EAGT Mchungaji Dr Brown Mwakipesile katika adhimisho la Ibada Kuu ,Mch Andrea Haule wa kanisa la EAGT Chamwino Ikulu amesema watu wengi wamekuwa wakiteswa na nguvu za giza kutokana na kutegemea nguvu zao ana akili zao katika mang,amuzi mbalimbali.
“Mtakeni Bwana na nguvu zake ,tafuteni uso wa Mungu siku zote ,hujui shetani amewaza nini ,na lazima ufahamu tangu umeokoka umetangaza vita naye,ni muhimu kumtafuta Mungu katika ulimwengu wa mwili na roho,ili kupata mabadiliko ya ndani”Amesema
Mch.Haule amesema kuwa kama msingi wa kanisa ulivyowekwa ile siku ya pentekoste pale ambavyo roho aliwajaliwa na wakazungumza na kunena kwa lugha mbalimbali ,ikumbukwe kwamba ndio msingi ambao waamini wanapaswa kuufuata ili kuweza kuyaishi matakatifu ya Mungu na kiulimwengu na kuyashinda ili kuitenda ile kazi ya Roho Mtakatifu aliyeachiliwa ndani ya waamini.
“Ukaja kama upepo ,ukawashangaza wote nao wakatikiswa nayo ilikuwa ahadi ,yao,sasa sisi tumekosa hiyo je tufanyaje ,unajua jambo linalotikisa ,n a tunaona uzoefu wa kanisa la kwanza na ndio ahadi yao ,na hao mitume ikawa hivyo na neema ya Mungu ikawa juu yao.”amesisitiza Mch.Haule
Hata hivyo Mch. Haule ameendelea kusema kuwa ili waamini waitende vema kazi ya Bwana na hawana budi kuishinda dhambi na kuishi katika hali ya utakatifu ni kama neno lake lisemavyo mtakeni Bwana na nguvu zake na mumtafute yeye siku zote ndivyo wataweza kuyatenda na kuyaishi katika hali ya unyenyekevu kama Yesu anavyotaka watu wake waishi.
“kama huna nguvu za Mungu utapataje kupona ,wewe ni shahidi wa kristo umeamka asubuhi umekuja kanisani ,kwanini uteswe na nguvu za giza ,ikiwa Yesu anaishi ndani yako,huna haja ya kuwa na hofu kwa kuwa tayari unao nguvu ya wokovu ndani yako.”Amesema .
Ibada Kuu ya Kanisa hilo kufanyika kila jumapili ya mwisho ya kila mwezi mwezi ,lengo likiwa ni kujumuika na waamini wanaokusanyika kwa pamoja kuabudu,kusifu maombezi ya wenye mahitaji mbalimbali huku ikipambwa na kwaya,mbalimbali ,shuhuda na kumtangaza Yesu Kwa Mataifa ili Wamjue na kuzitenda kazi zake katika Roho na Kweli.