******************************
Na Masanja Mabula, Pemba.
WAKAAZI wa shehia ya Sellemu Wilaya ya Wete wametakiwa kuwaepuka wanasiasa wanaotaka kuwatumilia vibaya kuchafua amani ya nchi katika kipindi hichi cha uchaguzi.
Sheha wa Shehia hiyo ndg, Ali Khatib Chwaya ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae Mwaka huu.
Amesema ni vyema kila mwananchi kwa mujibu wa nafasi aliyonayo kushiriki kutunza amani ya nchi ikizingatiwa kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi.
Aidha amewasisitiza wanasiasa kuendelea kuhubiri amani na kujiepusha na siasa za chuki na uhasama miongoni mwa jamii jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Sheha wa Shehia ya Sellem Ndg, Chwaya pia amewataka wananchi wenye sifa kujitokeza wenye vituo vya kupigia kura siku ikifika ili kutumia fursa yao kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaowataka.