……………………………………………………….
Mtama, Lindi
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amesema atawania tena nafasi ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo akiahidi kuwa Julai 14, 2020 atakwenda kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama (CCM) na ana imani kuwa atateuliwa, hivyo wananchi wamuunge mkono.
Nape amesema hayo leo Julai 3, 2020 wakati akizungumza na wananchi katika jimbo hilo la Mtama kuwashukuru kwa kuwa pamoja kwa kipindi cha miaka mitano wakifanya kazi kwa pamoja hataua ambayo alisema imeleta mafanikio katika jimbo hilo.
Katika Mkutano huo Nape ametumia nafasi hiyo kuelezea maendeleo ambayo yamefanyika katika jimbo la Mtama chini ya uongozi mahiri wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli akitolea mfano wa barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Masasi.
“Barabara kutoka Mtwara mpaka Masasi imepatikana kwa sababu Rais alibana matumizi, pia amerudisha heshima ya utumishi na ndio maana mpaka leo unawasikia watumishi wanalalama vyuma vimekaza, unajua maana yake nini hakuna semina, hakuna posho