Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu,akizungumza wakati wa utoaji wa daraja za nyota kwa hoteli zilizopangwa katika daraja za ubora Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda akizungumza kwenye hafla ya utoaji Nyota kwenye hoteli zilizokidhi vigezo iliyofanyika leo Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akitoa ngao ya mshindi wa hoteli ya nyota tatu leo Katika utoaji wa daraja za nyota kwa hoteli zilizopangwa katika daraja za ubora Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akitoa ngao kwa mshindi wa hoteli ya Nyota tatu leo katika utoaji wa daraja za nyota kwa hoteli zilizopangwa katika daraja za ubora Jijini Dodoma.
Washindi wa Hoteli za Nyota tatu za Jijini Dodoma(waliyo simama nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu leo Katika utoaji wa daraja za nyota kwa hoteli zilizopangwa katika daraja za ubora Jijini Dodoma.
……………………………………………..
Na.Majid Abdulkarim, Dodoma
Wamiliki wa Hoteli za Kitalii Nchini watakiwa kutoa huduma bora na kuboresha huduma zao ili kuwahakikishia watalii wako salama wakiwa nchini kwa kuongeza ushawishi kuendelea kuja kufanya utalii Tanzania.
Wito huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu leo Katika utoaji wa daraja za nyota kwa hoteli zilizopangwa katika daraja za ubora Jijini Dodoma.
Mhe.Kanyasu amesema kuwa kukosekana mpangilio husio mzuri wa kitaalam juu ya kuaanda hoteli na kutumia wahudumu wasio kuwa na taaluma husika katika mahoteli ni mambo muhimu wamiliki watakiwa kuyafanyia kazi ili hoteli hzio kukidhi vigezo vya kupokea watalii.
Aidha Mhe. Kanyasu amesema kuwa wamiliki wote wanatakiwa kutoa huduma bora kwa watalii zitakazo endana na gharama ya fedha wanayowatoza katika kuwapangisha maradhi watalii ili kuongeza ushawishi kwa watalii kuendelea kuja kwa wingi nchini.
“Wamiliki wa Hoteli lazima muwe wabunifu kwa kushirikisha watu wa mipango miji, wataalamu wa afya, watu wa miundo mbinu na watu wengine muhimu kwenu ili kuhakikisha hoteli zinazojengwa zinakidhi vigezo vyote vya kupokea watalii na kuendana na madaraja tuliyonayo hapa nchini”, amesisitiza Mhe. Kanyasu.
Mhe. Kanyasu mameendelea kusema kuwa wamiliki hao wanatakiwa kufanyia kazi mapungufu madogo madogo katika hoteli zao kama wataalamu wamadaraja ya ubora wa hoteli walivyo washauri na kuwaelekeza ili kufikia ubora na vigezo vilivyo ainishwa ili kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri na kuboresha huduma za maradhi katika jiji letu la Dodoma.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda ameeleza wizara imejipanga kikamilifu kutambua kila ya aina ya huduma katika hoteli kwa kutumia mfumo wa Elekitloniki ili kuweza kutoa daraja za ubora wa hoteli kwa ufasaha
“Wamiliki biashara ya utalii inatakiwa kupewa kipaumbele kwani sekta ya utalii nchini imekuwa chachu ya kuongeza pato la taifa kutokana na watalii wengi kuja nchini kufanya utalii”, amesema Prof. Mkenda
Katika hafla hiyo ya utoaji wa madaraja ya nyota kwa hoteli zilizopangwa katika daraja za ubora Jijini Dodoma Hoteli tatu tu ndo zimepata daraja la Nyota Tatu, hoteli mbili zikipata Daraja la Nyota Mbili na Hoteli Nyingine kupata daraja D na A .
Hoteli hizo zimekidhi vigezo kwa madaraja ya nyota mbili na D na A na kutunukiwa vyet huku hoteli za nyota tutu zikitunukiwa vyeti na ngao ambazo ni Fantacy Village, Hotel ya Nashera na New Dodoma Hoteli.