Mkurugenzi wa uendeshaji UTT-AMIS Issa Wahichindena akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha kuhudumia wawekezaji cha UTT-AMIS katika jengo la Ngorongoro, jijini Arusha, anayeangalia (Katikati) ni meneja wa uhusiano katika kitengo cha uangalizi wa amana katika benki ya CRDB, Mary Mponda (Picha na Pamella Mollel)
Meneja wa Uhusiano, kitengo cha uangalizi wa amana, katika Benki ya CRDB Mary Mponda (Kulia), akizungumza katika uzinduzi wa UTT Arusha, huku Meneja wa Tawi la TFA la benki ya CRDB Arusha Ronald Paul (Kushoto) akifuatilia kwa makini (Picha na Pamella Mollel)
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Daudi Mbaga akizungumza na waandishi wa habari wa kati wa hafla hiyo (Picha na Pamela Mollel)
Picha ya Pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa UTT-AMIS na wafanyakazi wa benki ya CRDB mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kuhudumiawawekezaji Arusha (Picha na Pamella Mollel).
**********************************
Kampuni ya Serikali inayohusika na Uanzishaji na Uendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini, UTT-AMIS imezindua tawi lake la tatu jijini Arusha baada ya lile la Dodoma katika mkakati wake wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
“Tunafungua rasmi kituo cha kuhudumia wawekezaji wetu katika jiji la Arusha, hii ni ikiwa ni ushahidi wa maendeleo mazuri katika sekta ya uwekezaji kwa wananchi wa kawaida, Tanzania zikiwa ni juhudi kubwa za serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Maguifuli,” alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji wa UTT-AMIS, Issa Wahichindena.
Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho katika jengo la Ngorongoro Conservation Center, lililopo katikati ya jiji, Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kwa kuwekeza katika mifuko hiyo wawekezaji wananufaika na unafuu wa gharama za uwekezaji.