Home Mchanganyiko WAKIMBIZI 176 WA BURUNDI WAREJEA KWA HIARI NCHINI KWAO LEO BAADA YA...

WAKIMBIZI 176 WA BURUNDI WAREJEA KWA HIARI NCHINI KWAO LEO BAADA YA AMANI NA USALAMA KUREJEA KWENYE NCHI YAO

0

Mkuu wa Msafara uliowasindikiza Wakimbizi wanaorejea kwa hiari Burundi, ambaye ni Afisa Tawala wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Ngeze Ramadhani (Kulia). Akimkabidhi Mwakilishi wa Serikali ya Burundi Jules Bagayimpunzi (Kushoto), Nyaraka zinazowahusu Wakimbizi 176 waliorejea kwa hiari Nchini Burundi. Tukio hilo limefanyika leo katika Mpaka wa Tanzania na Burundi Manyovu Mkoani Kigoma na kuwashirikisha Serikali ya Tanzania, Burundi na Mashirika ya Kimataifa yanayohudumia Wakimbizi.

Mratibu wa Usalama wa UNHCR Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, Cathie Monni (Kushoto), akibadilishana na Mwakilishi wa UNHCR Kigoma Nyaraka zinazohusu Wakimbizi wa Burundi 176 waliorejea Burundi leo kutoka Tanzania. Tukio hilo limefanyika leo katika Mpaka wa Tanzania na Burundi Manyovu Mkoani Kigoma na kuwashirikisha Serikali ya Tanzania, Burundi na Mashirika ya Kimataifa yanayohudumia Wakimbizi. 

 Baadhi ya wawakilishi wa Serikali ya Burundi na Watumishi wa Mashirika yanayohudumia Wakimbizi Nchini Tanzania, Wakiwatazama Wakimbizi waliomo ndani ya mabasi  manne waliyokuwa wakisafiria kutoka Nchini Tanzania kurejea kwa hiari Nchini kwao Burundi. Tukio hilo limefanyika leo katika Mpaka wa Tanzania na Burundi Manyovu, Mkoani Kigoma na kuwashirikisha Serikali ya Tanzania, Burundi na Mashirika ya Kimataifa yanayohudumia Wakimbizi.

Baadhi ya wawakilishi wa Serikali ya Burundi na Watumishi wa Mashirika yanayohudumia Wakimbizi Nchini Burundi, wakiwa tayari kuwapokea  Wakimbizi 176 wa Burundi waliorejea kwa hiari nchini kwao leo. Tukio hilo limefanyika katika Mpaka wa Tanzania na Burundi Manyovu, Mkoani Kigoma na kuwashirikisha Serikali ya Tanzania, Burundi na Mashirika ya Kimataifa yanayohudumia Wakimbizi.