Home Teknolojia UDSM WATENGENEZA KIFAA TIBA (NEONATAL INCUBATOR) KUOKOA WATOTO WACHANGA

UDSM WATENGENEZA KIFAA TIBA (NEONATAL INCUBATOR) KUOKOA WATOTO WACHANGA

0

Kifaa tiba (Neonatal Incubator) ambacho kipo kwaajili ya kumsaidia mtoto mchanga ambaye amezaliwa akiwa na matatizo ya kiafya. Mkufunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Mhandisi Majili Killo akimuelezea mteja aliyetembelea banda la maonesho la chuo hicho katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia kurugenzi ya ubunifu na ujasiliamali (UDIEC) wametengeneza kifaa tiba  (Neonatal Incubator) kwaajili ya kumsaidia mtoto mchanga mwenye matatizo ya kiafya baada ya kuzaliwa 

Akizungumza katika maonesho ya 44 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam Mkufunzi UDSM,Mhandisi Majili Killo amesema wameamua kutengeneza kifaa tiba hicho ili kuweza kusaidia watoto hasa katika vituo vidogo vya afya ambavyo haviwezi kupata mashine hiyo kwa urahisi.

Amesema kuwa Kurugenzi ya Ubunifu na Ujasiliamli iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unahifadhi vijana wabunifu na wajasilimali kufikia ndoto zao

“Mimi pamoja na wanafunzi wangu tulikuwa na ndoto ya kutengeneza kifaa hiki maalumu ( Neonatal Incubator ) kwaajili ya watoto wadogo wanapozaliwa siku 0 hadi 28 na zaidi ya hapo inawezekana amezaliwa kabla ya siku (Watoto njiti) au wamezaliwa kawaida lakini akapata shida ya changamoto ya afya”. Amesema Mhandisi Killo.

Aidha Mhandisi Killo amesema kifaa tiba hicho hakina gharama pia kinaweza kutumika mahali ambapo umeme unatumika wa sola,jenereta au betri.

Pamoja hayo Mhandisi Killo amesema kifaa tiba hicho kinauwezo wa kuangalia mwenendo wa moyo wa mtoto kama unamatatizo.

Hata hivyo Mhandisi Killo amesema lengo la kutengeneza kifaa tiba hicho ni pamoja kuokoa gharama pia kusaidia vituo vidogo vya afya kuweza kupata kifaa tiba hicho kwaajili ya kumlinda mtoto.