MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, huko Mahonda.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,akiwasisitiza Wajumbe hao kusoma kwa kina Kanuni za uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM.
Katibu wa Chama Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa huo, Mulla Othman Zubeir,akisoma taarifa za kazi za CCM Mkoa huo.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakifuatilia nasaha zinazotolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan, huko Mahonda Unguja.
*****************************
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi na wanachama wa CCM Mkoa huo kuweka mbele maslahi ya Chama badala ya maslahi yao binafsi.
Hayo ameyasema katika mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha Chama, wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, huko katika Ofisi za Chama Mahonda.
Alisema kila kiongozi anatakiwa kutekeleza wajibu wake kwa kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi mkuu wa dola wa mwaka huu.
Mhe.Samia aliwambia wajumbe hao kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kiuongozi hivyo wanatakiwa kuwa mfano bora kwa wanachama wanaowaongoza.
” Tufanyeni kazi kwa upendo,ushirikiano na uadilifu mkubwa kwa lengo la kuhakikisha Chama kinashinda kwa asilimia kubwa na kulinda heshima ya Mkoa huu.”, alisema Mhe.Samia.
Katika maelezo yake Mhe.Samia,alisema kila mwana CCM anatakiwa kulinda kwa vitendo tunu za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na Muungano kwa kuhakikisha CCM inashinda na kubaki madarakani.
Kupitia kikao hicho Mhe. Samia, aliwapongeza viongozi wa mkoa huo kwa mabadiliko makubwa yaliyofikiwa katika kuimarisha chama na kuwasihi walinde heshima hiyo kwa kukiletea ushindi chama katika uchaguzi.
Naye Katibu wa Chama Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa huo, Mulla Othman Zubeir, alisema chama kimejipanga vizuri kuhakikisha kinashinda katka uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mulla alisema, ndani ya mkoa huo Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 imetekelezwa kwa asilimia 99 katika sekta za elimu na afya.
Aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ndani ya Mkoa huo.