**************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda amewapatia kazi TAKUKURU ya kuchunguza 10% ya pesa zinazotolewa na Serikali kwaajili ya kukwamua Wanawake,Vijana na walemavu Kama zimewafikia walengwa na kutoa majibu kabla ya tarehe 20 mwezi wa 7 mwaka huu.
Hayo ameyazungumza leo wakati wa kukabidhi miradi iliyopo katika Wilaya ya Ubungo alipokuwa akikagua vikundi vya ujasiliamali vilivyopata mkopo kutoka Serikalini .
“Serikali imetoa Bilioni 33 kwaajili ya kukwamua wamama,walemavu na vijana sina uhakika kama fedha hizo zinawafikia walengwa TAKUKURU fanyeni uchinguzi na majibu yapayikane kabla ya July 20 mwaka huu”amesema RC Makonda.
Pia amesema kuanzia leo July 1 Mkoa wa Dar es Salaam umerudi rasmi kwenye shughuli zake za kawaida watu wafanye kazi na wamiliki wa hoteli,baa,kumbi na biashara mbalimbali watembee kifua mbele kwasababu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mchamungu zipo nchi mpaka sasa wanajifungia ndani kwaajili ya janga la Corona.
Vilevile Rc Makonda amekabidhi miradi mingine kama upanuzi wa barabara kutoka Shukikango kwenda Bamaga yenye urefu wa km 3.7 ,upanuzi wa hospitali ya Palestina ambayo itakuwa ya ghorofa 4 itakayoweza kuhudumia wagonjwa 2000 baada ya kukamilika .
Sanjari na hayo pia amekabidhi mradi wa mto ng’ombe ambao Ni miongoni mwa mito 8 mikubwa ya Jijini Dar es Salaam ambao utamwaga maji mto msimbazi na utaghalimu Bilioni 32 kukamilika.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Urafiki Motorcycle Group Husein Kamote ameishukuru Serikali kwa kuwapatia mkopo usio na riba ambao umewakwamua kimaisha .