Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akizugumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Maji Mhandisi Anthony Sanga,akizugumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini Mhandisi Nadhifa Kemikimba,akizugumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Dkt.George Lugomela,akizugumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa bodi ya Geuwasa kutoka Geita Bi.Patricia Kampambe akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange,akizugumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wakurugenzi na wenyekiti wa bodi za maji wakifatilia hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akiangalia utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira iliyofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amezitaka mamlaka za maji nchini kuwajali wateja wa maji na kuwahudumia inavyostahili kwa maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kuwa wabunifu katika utendaji wa kazi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Prof.Mkumbo wakati wa utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya maji na Bodi za maji za mabonde na mamlaka za maji safi na mazingira amesema kuwa baadhi ya Mamlaka zimekuwa na majibu yasiyofaa kwa wateja wa maji.
Prof.Mkumbo amesema kuwa kutokana na huduma au lugha mbaya kwa wateja, inapelekea wateja hao kumtafuta ili aweze kuwasaidia, jambo
ambalo haliko sawa.
“Zipo lugha ambazo mnawapa wateja zinatisha haikubalikia hata kidogo ,sasa kumbuka mishahara yako unayolipa wafanyakazi wako,kila kitu ni kwa sababu ya wateja hivyo unatakiwa kuwajali kwa sababu wewe umefundishwa namna ya kuwajali wateja”Amesema Prof.Mkumbo
Hata hivyo Prof.Mkumbo amesema kuwa ili kuondoa kero ya ukosefu wa
maji Wizara hiyo imezindua Gridi ya Taifa ya Maji kutoka katika vyanzo
vikubwa vya maji ili kusaidia maeneo ambayo hakuna vyanzo vya maji.
‘’Gridi ya Taifa ya Maji tayari tumeshaanza mradi wa maji kutoka
Ziwa Viktoria kwenda katika Mikoa ambayo kuna shida ya maji, ambapo
tayari Mikoa ya karibu na Mwanza wameanza kufaidika na mradi huo”amesisitiza Prof.Mkumbo
Hata hivyo Prof.Mkumbo amesema kuwa anatarajia kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo endapo atapitishwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambalo lilikuwa likiongozwa na Mbunge wa Chadema Mhe.Saed Kubenea.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga amewataka kushughulikia malalamiko ya wateja kuhusiana na Ankara za maji pamoja na kutumia lugha nzuri ili kuwahudumia bila matatizo.
Kwa upande wake Mkurungezi idara ya Rasilimali za maji Dkt Genge Lugomela akitoa taarifa za mikataba ya utendaji maji wa bodi za maji za Mabonde kwa mwaka 2019/20 amebainisha kuwa kila bodi ya maji ya bonde inatakiwa kutumia asilimia 30 ya mapato yake.
“Maswala ya ukusanyaji wa takwimu za rasilimali za maji Yanapatiwa fedha kwa maana ya kuendesha vituo na kuhakikisha kuwa takwimu za rasilimali za maji zinapatikana kwa wakati lakini pia wadau wote wanapata takwimu hizo.”amesema Dkt.Lugomela
Naye Mkurungezi idara ya usambazaji maji Mhandisi Nadhifu Kemikimba amesema kuwa zoezi hilo linahusisha mamlaka za maji 69 na katika mamlaka hizo mamlaka za miji mikuu ya mikoa ni 26 na mamlaka za miradi ya kitaifa zilikuwa nane lakini sasa zimebaki saba baada ya chaliwasa kuunganishwa na dawasa.
“kwa hiyo kwenye national project ziko saba ambazo zitasaini leo ,lakini pia mijoi midogo zitasaini miji 26 ,na tuna miji ambayo iko chini ya usimamizi wenyewe hawana bodi kwa wamewekwa kwenye bodi zingine,kwa hiyo mwenyekiti wa bodi atasaini kwa niaba ya bodi hizo”amesisitiza Mhandisi Kemikimba
Baadhi ya wenyeviti wa bodi za mamlaka za maji kutoka Mikoa mbalimbali Nchini wameahidi utekelezaji unaostahili na kuipongeza wizara ya maji kupitia mpango wake wa kupeleka maji katik vituo vya afya na shuleni.