………………………………………………………….
Na.Mwaandishi Wetu,Dar es Salaam
Sasa rasmi ni Yanga na Simba Nusu Fainali ya Kombe la Azam Sports Federation baada ya wekundu wa Msimbazi kuwachapa mabao 2-0 matajiri wa Chamazi Azam FC mchezo uliomaliza katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ni mechi ya kisasi Simba itataka kulipa deni la kufungwa na Yanga Machi 8 mwaka huu mchezo wa Ligi Kuu mbele ya Rais Dkt.John Magufuli bao ambalo lilifungwa na Bernad Morrson.
Au utakuwa mwaka wa Yanga kuitesa Simba baada ya mechi ya kwanza kutoka sare ya mabao 2-2 mchezo wa Ligi Kuu na mechi ya pili Mnyama kufungwa 1-0.
Mabao yaliyoipeleka Simba Nusu Fainali yamefungwa na John Bocco dakika ya 39 akipokea pasi ya Kahata na Clatous Chama alifunga bao la pili dakika ya 56 akimalizia pasi ya Shomari Kapombe.
Yanga wao walitinga jana baada ya kuichapa 2-1 Kagera Sugar na Nusu Fainali ya pili itakuwa ni Namungo FC na Sahare Stars ambayo imeitoa Ndanda FC kwa njia ya matuta.