Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM, waliofika Makao Makuu ya chama hicho, Jijini Dodoma kuhushudia alipokuwa akirejesha fomu za udhamini wa kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya ya CCM kugombea Urais wa Tanzania Oktoba 2020. Katika mkutano alitumia fursa ya kuwashukuru wanachama wote waliomdhamini na kwamba ana deni kubwa kwao. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDAMwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeries akikabidhi kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli fomu za wanachama waliomdhamini wa mkoa huo. Picha zingine ni wenyeviti wa CCM wa mikoa wakikabidhi fomu za udhamini kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli ambaye alirejesha fomu za kuomba kugombea urais wa Tanzania kupitia cha chama hicho.Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Magufuli akiwa na viongozi wa chama hicho wakiwemo viongozi wa Jumuiya za chama hicho.
*******************************
Na Richard Mwaikenda,Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amewashukuru sana wote waliojitokeza kumdhamini kwa kujaza fomu za kuomba kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020, kupitia chama hicho.
Shukrani hizo alizitoa mara baada ya kurejesha fomu Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma, ambapo kwa kitendo hicho cha kudhaminiwa na zaidi ya wanachama milioni moja wa Tanzania Bara na Visiwani, amesema kinamfanya awe na deni kubwa kwao.
Pia, Dk. Magufuli aliwapongeza Wenyeviti wa CCM wa mikoa yote 32 kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kufanikisha udhamini huo mkubwa, licha ya kupata lawama nyingi kwa waliojitokeza kudhamini lakini walikosa fursa hiyo.
Aliwaomba wanachama waliokuwa na nia hiyo, wasivunjike moyo bali udhamini huo wauweke kwenye kura endapo mikutano husika ya chama itampitisha kuwa mgombea urais wa Tanzania kupita chama hicho, ili akapambane na wagombea wa vyama vingine.
Pia aliwaomba wanachama wa vyama vingine wampigie kura wakati wa kinyang’anyiro hicho, ili awatumikie Watanzania kutimiza malengo waliyojiwekea pamoja na kukamilisha miradi mbalimbali waliyoianza katika Serikali ya Awmu ya Tano inayoongozwa na yeye, ikiwemo ya Reli ya Kisasa ya Mwendo Kasi (SGR), Mradi mkubwa wa umeme wa Mwalimu Nyerere Rufiji na miradi mingine mingi.
Kabla ya kurejesha fomu, lilifanyika tukio la wenyeviti wa mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani kukabidhi fomu za waliomdhamini kutoka katika mikoa hiyo. Pi wenyeviti wa Jumuiya za chama hicho; Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Umoja wa Wazazi Tanzania na Umoja wa Vijana (UVCCM), walikabidhi fomu za waliomdhamini Dk. Magufuli.