Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba ,kamishna Msaidizi Mwandamizi Juma Sadi Khamis akizungumza na mwandishi wa habari juu ya tukio la wizi wa taa za barabarani katika mji wa Wete.
Picha na Masanja Mabula
Na Masanja Mabula,PEMBA..
IKIWA ni siku tisa tangu Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dkt Ali Mohammed Shein kutaka waliohusika na wizi wa taa za barabarani katika mji wa Wete kujisalimisha kwenye vyombo vya sheria, tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linawashikili watu wawili wanaotuhumiwa kuhisika na tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishna Msaidizi Mwandamizi Juma Sadi Khamis akizungumza ofisini kwake alisema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
Kamanda Sadi alisema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na doria zinazoendelea kufanya na shauri hilo litapelekwa kwa Mkurugenzi wa mashtaka wa serikali.
“Bado tunaendelea kuwahoji watuhumiwa na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani”alisema.
Aidha Kamanda Sadi aliwataka wananchi kushirikiana na askari shehia kwa kuwapa taarifa sahihi na hii inajenga dhana ya ulinzi shirikishi.
“Katika shehia tunaaskari shehia ambaye ni katibu wa kamati ya ulinzi ,hivyo tunaomba sana wawape ushirikiano ili kuweza kuwfichukua wanaohusika na vitndo vya kihalifu”alisisitiza
Katika hatuba yake wakati akilivunja baraza la wawakilishi , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Ali Mohamed Shein alielezea kutoridhishwa na kitendo cha kuibwa taa za barabarani katika Mji wa Wete.