Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine wa Chama cha Mapinduzi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula, Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally Kakurwa mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa NEC katika Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya Ukumbi wa NEC mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kurudisha Fomu ya Maombi ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuzijaza Fomu hizo na kupita wadhamini katika mikoa yote ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha na kusaini Fomu za maombi ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuzijaza Fomu hizo na kupita wadhamini katika mikoa yote ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Fomu zake alizopata wadhamini mara baada ya kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika Ukumbi wa NEC makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ukumbi wa NEC wa Chama cha Mapinduzi mara baada ya kurudisha Fomu zake.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama mbalimbali wa CCM waliokusanyika nje ya Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma mara baada ya kurudisha Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Sekretariet ya Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuzungumza katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wanachama wa CCM mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama White House jijini Dodoma. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais John Magufuli, ambaye ni mgombea urais kupitia chama hicho amerudisha fomu za kugombea nafasi hiyo leo Juni 30, 2020, jijini Dodoma, katika ofisi kuu za chama hicho.
Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 17 mwezi huu Rais aliweza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kuwa Rais katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo Rais Magufu amevunja rekodi ya kupata kudhaminiwa na wanachama 1,023,911 Tanzania nzima.
Kikao cha Kamati Kuu kitakaa Julai 10, 2020, ili kupitisha majina ya wagombea urais, Tanzania na Zanzibar.
Mkoa wa Morogoro umevunja rekodi kwa mikoa yote 32 kwa kumpatia udhamini mkubwa na wa kishindo ni wanachama 117,450,Geita wanachama 89,595,Mara wanachama 87,550,Dar es salaam wanachama 71,491,Tanga wanachama 62,839 hiyo ni baadhi ya mikoa iliyomdhamini Rais kwa idadi kubwa ya wanachama.
Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania, UWT wanachama 66,633 wamejitokeza pia kumdhamini Rais Dkt.Magufuli,Jumuiya ya Wazazi ya CCM wanachama 48,329 nao wamejitokeza kumdhamini Rais Dkt.Magufuli huku Jumuiya ya Vijana wanachama 103,063 nao wamejitokeza kumdhamini Rais Dkt.Magufuli
Katika hatua nyingine katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt.Bashiru Ally,amesema kuwa kuanzia kesho Tarehe Moja, nafasi za Ubunge na Udiwani zipo wazi. Wanachama wenye sifa kesho waanze kupita kwenye Ofisi kuulizia utaratibu.