Diwani wa kata ya Chamwino Jumanne Gende akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Bonaza kabla ya Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde ambaye amekabidhi mabati na nguzo za chuma vyenye thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Bonaza pamoja na kuboresha miundo mbinu.
Katibu wa Soko la Bonaza Bw.Dickson Pastory akisoma taarifa kwa Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde ambaye amekabidhi mabati na Nguzo za Chuma katika Soko la Bonaza vyenye thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Bonaza pamoja na kuboresha miundo mbinu.
Katibu wa Soko la Bonaza Bw.Dickson Pastory akimkabidhi risala Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde ambaye amekabidhi mabati na Nguzo za Chuma katika Soko la Bonaza vyenye thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Bonaza pamoja na kuboresha miundo mbinu.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Bonaza kata ya Chamwino ambapo amekabidhi Mabati na Nguzo za Chuma yakiwa na thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo pamoja na kuboresha miundo mbinu.
Sehemu ya wafanyabiashara wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde ambaye amekabidhi Mabati na Nguzo za Chuma katika Soko la Bonaza yakiwa na thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Bonaza pamoja na kuboresha miundo mbinu.
Meneja wa tawi la Dodoma kutoka ALAF Bw.Grayson Mwakasege akizungumza wakati wa Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akikabidhi Mabati na Nguzo za Chuma katika Soko la Bonaza yakiwa na thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Bonaza pamoja na kuboresha miundo mbinu.
Meneja wa tawi la Dodoma kutoka ALAF Bw.Grayson Mwakasege akimkabidhi Mabati Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kisasa la Bonaza katika Kata ya Chamwino wilayani Dodoma mkoani Dodoma.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akiwa na wafanyabiashara wakiwa wameshika nguzo za chuma kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kisasa la Bonaza lililopo Kata ya Chamwino wilayanio Dodoma.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akinunua bidhaa mbalimbali mara baada ya kukabidhi Mabati na nguzo za Chuma kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kisasa la Bonaza lililopo Kata ya Chamwino wilayani Dodoma yakiwa na thamani ya Milioni 25.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akikabidhiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa Soko la Bonaza mara baada ya kukabidhi Mabati na nguzo za Chuma kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kisasa la Bonaza lililopo Kata ya Chamwino wilayani Dodoma yakiwa na thamani ya Milioni 25.
………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mbunge wa Dodoma Mjini , Anthony Mavunde amekabidhi mabati 400 na mabomba vyote vikiwa na thamani ya Milioni 25 ili kuboresha miundo mbinu ya Soko la Bonanza lililopo kata ya Chamwino wilaya ya Dodoma Mkoani Dodoma.
Hatua hiyo imefikiwa leo katika kukamilisha ahadi aliyoitoa haadi 2015 kipindi alipokuwa akiomba dhamana ya kuwa mbunge wao na leo katimiza ahadi hiyo.
Aidha Mavunde amasema kuwa upatikanaji wa mambomba na mabati hayo ya kuezeka eneo lililo kuwa wazi katika soko hilo linafanya soko hilo kufikia asilimia 80 katika kukamilisha ukarabati huo ili wakazi wa maeneo hayo kufanya biashara zao katika mazingira safi na salama kwa wateja wao.
Mavunde amesema kuwa hilo soko linatakiwa kuwa la kisasa kutokana na Dodoma ni makao makuu ya nchi hivyo kila kitu kwa Dodoma kinatakiwa kuwa kivutio kikubwa kwa wageni watakaokuja kutembea.
”Hili Soko litakuwa tofauti na masoko mengine ambayo nimeyajenga kutokana hili ni hatua ya mwisho nitajenga tofauti kwa kuwawekea na TV kubwa ambapo mtakuwa mnaangalia taarifa ya habari na vipindi mbalimbali huku mkifanya biashara zenu”amesema Mavunde
Pia ametoa shukrani za dhati kwa uongozi wa soko hilo kwa uvumilivu waliyompa ili kukamilisha ahadi hiyo na sasa leo amekamilishwa.
“katika kufanya kazi lazima viongozi mshirikiane kwa ukaribu ili kutekeleza dhamana ya kuwa kiongozi hivyo ndivyo uongozi wa soko wamenipa ushirikiano mpaka leo natimiza haadi niliyo toa 2015”, amesema Mavunde.
Mavunde ametoa wito kwa wakazi hao na kusema kuwa sasa ni wakati wa kufumbua macho yeyote anayekuja katika ulingo wa siasa aje na siasa ya maendeleo kwa watu wake ndo dhamana ya uongozi wa sasa katika siasa ilivyo.
“2015 Mlipo nipa dhamana ya kuongoza nilikuwa najifunza uongozi sasa nimeiva ni wakati wa kufanya kazi kama Mbunge hivyo ni mwendo wa kutekeleza kwa vitendo dhamana mtakayonipa panapo majali muda ukifika hapo Oktoba mwaka huu”, amesma Mavunde.
Mavunde ameongeza kuwa kauli ya kutekeleza kwa vitendo ni kutokana na mfumo wa Mhe. Rais Dkt. Magufuli ya kutimiza adhima aliyopewa na wananchi kwa kugusa Maisha ya kila wananchi wa kawaida hivyo sisi kama wasaidizi wake jukumu kubwa ni kutafasiri maelekezo yake ili kumkomboa mwanachi wa kawaida kuinua kipato chake na kutengeneza maendeleo yatakayo jenga taifa hili.
Naye Katibu wa Soko hilo Bw.Dickson Pastory ametoa ombi kwa mbunge huyo kuwawezesha wakazi wa Bonanza kupata stendi ya daladala ili kuongeza mzunguko wa pesa katika eneo hilo
“tunaomba jiji kurejesha ushuru wa soko kwani tumekuwa hatupati huduma za usafi kama kuondoshewa taka ambazo zimekuwa kero kwa wafanya biashara wa hapa”, ameeleza Bw.Pastory
Huku Meneja wa tawi la Dodoma kutoka ALAF Bw.Grayson Mwakasege ameeleza kuwa walipata ombi kutoka kwa mbunge juu ya mahitaji ya mabati alituma timu ili kujua ni aina gani ya mabati yanatakiwa na leo wamekuja na Mbunge kukabidhi mabati hayo.
Baadhi ya wafanyabiashara soko la Bonanza wameshukuru sana kupatiwa vifaa vya kuboresha soko ni faraja kwao kwani walikuwa wakifanya biashara chini ya jua huku wakinyeshewa mvua ila kukamilika kwa ujenzi huo itakuwa wanafanyabiashara kwa uhuru.