………………………………………………………………………..
Na Silvia Mchuruza,Bukoba.
Meli ya MV Victoria inatarajiwa kuanza safari yake ya majaribio june 28 mwaka huu baada ya kusimama kwa muda mrefu ikiwa kwenye matengenezo jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisi kwake mkuu wa mkoa wa Kagera Brig.Jen Marco E Gaguti amesema kuwa meli hiyo inatajiwa kutia nanga siku ya jumapili majira ya saa nane mchana katika bandari ya Bukoba ikitokea Mwanza ilikokuwa ikifanyiwa matengenezo makubwa ambapo safari hiyo ya majaribio itakuwa ya kwanza ya umbali mrefu baada ya safari fupi za majaribio kufanyika na kuonekana iko vizuri.
RC Gaguti amesema kuwa safari hiyo haitakuwa na abiria ila Mh. Rais ameridhia abiria kusafirisha mizigo yao kutoka bukoba kwenda mwanza bure ikiwa ni motisha kwa wakazi wa Bukoba na Mwanza ambao meli hii imekuwa kiunganishi kizuri cha kusafirisha mizigo kutoka Bukoba kwenda Mwanza kwa urahisi ambapo amesema kuwa baada ya safari hii ya majaribio kufanyika serikali itakuwa tayali kukabidhiwa meli hiyo kwa ajiri ya kuendelea na safari zake kama ilivyokuwa hapo awali.
Aidha RC Gaguti ametoa wito kwa wanachi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya jumapili bandarini kwa ajiri ya kuja kuipokea meli yao na kuiombea ili iweze kuanza safari zake salama kama kawaida.