Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya utoaji wa vyeti na zawadi kwa washindi wa shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango, iliyofanyika katika makao makuu ya shirika hilo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango, Bi.Luciana Makundi akizungumza katika hafla ya utoaji wa vyeti na zawadi kwa washindi wa shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango, iliyofanyika katika makao makuu ya shirika hilo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa uandaaji wa viwango wa shirika la viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema akizungumza katika hafla ya utoaji wa vyeti na zawadi kwa washindi wa shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango, iliyofanyika katika makao makuu ya shirika hilo Ubungo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akiwatunuku vyeti vya ushindi washindi wa shindano la la uandishi insha juu ya maswala ya viwango.
Mshindi wa kwanza shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango Bi.Herieth Alexander akionesha cheti alichotunukiwa kama mshindi wa shindano hilo katika hafla ya utoaji vyeti kwa washindi lililofanyika leo Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania TBS, Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa kwanza wa shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango Bi.Herieth Alexander akipata picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya katika hafla ya utoaji wa vyeti na zawadi kwa washindi wa shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango, iliyofanyika katika makao makuu ya shirika hilo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya (katikati mwenye miwani) akipata picha ya pamoja na washindi wa shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango.
********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Iwapo utaratibu wa kuandaa viwango utahusisha jamii,kisha matakwa yake yakazingatiwa katika nyanja zote husika, viwango vitakuwa na mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya changamoto wanazokumbana nazo wakimbizi.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya katika hafla ya utoaji wa vyeti na zawadi kwa washindi wa shindano la uandishi insha juu ya maswala ya viwango, iliyofanyika katika makao makuu ya shirika hilo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt.Ngenya amesema pamoja na kwamba viwango vyenyewe hutayarishwa kwa uwazi na ushirikishwaji, lakini pia huweka misingi ya uwazi katika mainisho yake.
“Mainisho yake huweza kutumika na taasisi mbalimbali za udhibiti kutengeneza kanuni zinazosimamia masuala mbalimbali katika jamiiyahusuyo ubora,usalama,afya,ulinzi wa mazingira,biashara na hata uadilifu katika utendaji”.Amesema Dkt.Ngenya.
Aidha, Dkt.Ngenya amesema kuwa tatizo la wakimbizi linaathiri maendeleo ya nchi nyingi za Afrika kutokana na kupunguza sehemu kubwa ya nguvu kazi katika maeneo ambayo wakimbizi wengi wanatokea.
“Uwepo wa wakimbizi umekuwa ukisababisha athari hasi kwa nchi wanazokimbilia ikiwa ni pamoja kuathiri usalama”. Amesema Dkt.Ngenya.
Pamoja na hayo Dkt.Ngenya amewapongeza Majaji pamoja na wanachuo mbalimbali walioshiriki katika shindano la uandishi wa insha kwani wamekuwa familia ya wanaviwango Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa maendeleo ya Taifa na Afrika kwa ujumla.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Shindano la uandishi wa Insha Bi.Luciana Makundi amesema muda wote walipokea insha 52 hawakufahamu ni nani amekusanya kwahiyo timu ilivyounda majaji watakaohusika waliletewa insha zenye namba moja hadi 52 na hawakufahamu ni nani ameandika wala ametoka wapi.
Pamoja na hayo Bi.Luciana ameishukuru TBS kwa kuwawezesha kushiriki shindano hilo muhimu wao kama walimu wanajifunza kutoka kwa wanafunzi wao hususani katika mada wanayofundisha kwani kwao ilikuwa ni fursa muhimu kupata mitazamo na mawazo kutoka kwa vijana wao kuhusu changamoto wanazokumbana nazo wakimbizi.
Nae Mshindi wa kwanza wa shindano hilo Bi.Herieth Alexander ameshukuru timu nzima iliyoshiriki shindano hilo pamoja na TBS kwani wamejifunza mengi hasa hususani changamoto wanazozipitia wakimbizi hapa nchini pamoja na bara la Afrika kwa ujumla.
Mshindi wa kwanza alifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi Milioni 1.5 pamoja na cheti.