Baadhi ya vibarua/wabeba mizigo katika bandari ya Bukoba wakiendelea na majumu yao ya kubeba na kupakia mizigo katika magari ya mizigo.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akiongea na wandesha boda boda wa Manispaa ya Bukoba akiwaeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuchangamkia fursa endapo meli itakapowasili mjini bukoba na kuanza safari zake za Bukoba –Mwanza.
Baadhi ya waendesha Pikipiki Manispaa ya Bukoba wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti katika viwanja vya Gymkhana Mjini Bukoba.
Muonekano wa meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU ikiwa katika bandari ya Mwanza tayari kwa kuanza safari ya majaribio ya kwenda Badari ya Bukoba juni 28,2020.
Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akionyesha tabasamu akifurahia kukamilika kwa ukarabati wa meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU itakayokuwa ikifanya safari zake kutoka Bukoba kwenda Jijini Mwanza baada ya Mhe. Rais John Magufuli kuamua meli hiyo ikarabatiwe.
Picha zote na Allawi Kaboyo.
………………………………………………………………………………
Na: Allawi Kaboyo Bukoba.
Wananchi mkoani Kagera na maeneo jirani watakiwa kujiandaa na fursa mbalimbali zitakazojitokeza baada ya meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU kuanza safari zake za Bukoba-Mwanaza ikiwa ukarabati wake umekamilika kwa asilimia 98% huku ikiwa imesimamisha safari hizo kwa takribani Zaidi ya miaka 3 kutokana na kuharibika.
Akitoa taarifa ya ujio wa meli hiyo leo Juni 26, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Bukoba, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujiandaa katika biashara na safari za kwenda mwanaza kwa kuwa mkombozi sasa anarejea.
Mkuu wa Mkoa Gaguti amesema kuwa meli hiyo itaanza kufanyiwa majaribio ya safari ndefu kwa mara ya kwanza ikitokea Jijini Mwanza na kuja bandari ya Bukoba juni 28,2020 ambapo haitaruhusiwa kubeba abiria Bali itabeba mizigo zaidi ya tani 100 na kuwataka wananchi wenye mizigo kujitokeza kwani wakati wa kurudi Mwanza itasafirishwa bure.
“Niombe kupitia kwenu wanahabari kuwaomba wananchi mkoani hapa kujitokeza kwa wingi ili kuipokea meli yao inayotarajia kuanza safari yake ya majaribio siku ya jumapili keshokutwa, ujio wa meli hii ni mapinduzi makubwa ya usafiri na usafirishaji katika ziwa Victoria chini ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe.Rais John Pombe Magufuli katika kuchochea uchumi wa wanankagera na watanzania kwaujumla.” Amesema Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Baada ya mkutano huo mkuu wa mkoa wa Kagera amepata fursa ya kuongea na waendesha pikipiki Maarufu kama (BODA BODA) Manispaa ya Bukoba juu ya ujio wa meli hiyo ambapo amesema kuwa wao kama wadau wa usafishaji wajiandae kwaajili ya kufanyakazi ya kuwasafirisha abiria pamoja na mizigo katika kipindi hiki cha ujio wa meli.
Abdusalum Mashankala ni mwenyekiti wa waendesha pikipiki manispaa ya Bukoba amesema ujio wa meli utaongeza mzunguko wa fedha kwa boda boda hao kwa kuwa watu watakuwa wengi watakao kuwa wanansafiri hivyo amewataka boda boda wenzake kujiandaa na fursa hiyo ambayo serikali imeamua kuirejesha.
Kwaupande wake meneja wa mamlaka ya bandari ndg.Bulenge Ndalo amesema mpaka sasa maandalizi ya kuipokea meli hiyo yanaendelea vizuri ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo na ofisi pamoja na kujenga godauni la kutunzia mizigo huku akiwaomba watanzania hasa wanakagera kuja kuwekeza katika biashara kwenye maeneo ya bandali.
“Nito wito kwa watanzania kuja kuwekeza kwakuwa tumejenga maeneo ambayo yanaruhusu kufanyia biashara kama migahawa na sehemu za kuuzia vinywaji hivyo fursa hii ipo na wakuitumia ni watanzania, kuanza kwa safari za meri kutatoa ajira hasa kwa vijana na tunatarajia kuanza na vijana 200 watakao kuwa wakifanya kazi kama vibarua na wafanyakazi wengine kama makarani.” Ameeleza Bw.Ndalo.
Vijana wa kubeba mizigo ni sehemu ya wadau muhimu katika badari hiyo kwaajili ya kubebea mizigo wao wamesema kuwa kuanza kwa safari za meli kutachagiza kukua uchumi wao wa kila siku ambao uliyumba kwa kiasi Fulani meli iliposimama.
Wameongeza kuwa baada ya meli kusimama baadhi yao walirudi vijijini lakini sasa watarejea kuanza kufanyakazi na kujipatia kipato huku wakiomba serikali kuwawekea utaratibu mzuri wa kuwawezesha kufanyakazi kwa usalama na Amani.