MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini
na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba akizungumza na washiriki wa semina maalumu kwa wasichana mkoani Tanga iliyoandaliwa na
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wanawake na Uongozi yenye makao
makuu yake Jijini Dar es Saalam
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini
na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na
Uongozi Shamira Mshangama
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini
na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba kushoto akimpongeza mmoja wa washiriki katika semina hiyo ambaye alitoa utenzi wake
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini
na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba kushoto akifurahi jambo na washiriki wa semina hiyo
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini
na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na
Uongozi Shamira Mshangama wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia Chama hicho Yosepher Komba na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na
Uongozi Shamira Mshangama wakiwa kwenye picha ya pamoja.
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba amewapa mbinu wanawake wanaotaka kuwania nafasi
za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi Octoba mwaka
huu hapa nchini ili kuweza kushinda kwenye maeneo yao.
Ametoa
mbinu hizo wakati akizungumza katika semina maalumu iliyoandaliwa na
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wanawake na Uongozi yenye makao
makuu yake Jijini Dar es Saalam ambapo alisema upo umuhimu wao
kuzingatia hayo iwapo wana dhamira ya dhati kutaka kugombea nafasi za
uongozi.
Semina hiyo ilishirikisha wajumbe wanawake kutoka vyama
vitano vyenye uwakilishi ambavyo ni Chadema, CCM, NCCR Mageuzi, ACT na
Chama cha Wananchi CUF ambapo aliwausia wajumbe hao kutambua kuwa
kampeni za uchaguzi sio rahisi na wanavyofikiria.
Yosepher
ambaye pia ni Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya
Kaskazini alizitaja
mbinu hizo ni rasilimali watu, muda, fedha na taarifa ya eneo husika
vitu ambavyo vikizingatiwa na mgombea yoyote anaweza kupata mafanikio
katika harakati zake za kisiasa.
“Ndugu zangu hizo ni
mbinu muhimu sana hasa unapotaka kusaka uongozi wa kisiasa hivyo
tambueni rasilimali watu mnapaswa kulipa kipaumbele sana kwani ndio
silaha ya ushindi na kuweza kuwafikisha kwenye mahali mnapotaka”Alisema
Makamu Mwenyekiti huyo.
Aidha aliwataka wanasiasa
wanawake mkoani Tanga kujiamini na kuchukua hatua pindi wanapojitokeza
kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufanikisha ndoto zao wa
kuwatumikia wananchi katika maeneo mbalimbali
Awali
akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na
Uongozi Shamira Mshangama alisema katika mafunzo ya siku mbili yalikuwa
yamejikita kuhamasisha wasichana walio ndani ya vyama vya siasa kuweza
kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu
ujao.
Alisema mafunzo hayo yameshirikisha vyama vitano ambapo
kila kimoja kimetoa wajumbe sita walikuwa na utayari wa kutia nia ya
kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao ikiwemo ubunge na
udiwani ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko kwenye jamii.
Mkurugenzi
huo alisema kwamba mradi huo wa “Nakataa Vikwazo Nagombea” unaendeshwa
na Shirika la Mwanamke na Uongozi ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Voice .