Home Mchanganyiko Zainab -ametoa rai kwa jamii kuacha kula ovyo bila mpangilio kujiepusha na...

Zainab -ametoa rai kwa jamii kuacha kula ovyo bila mpangilio kujiepusha na vitambi

0

**************************

24,Juni

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

OFISA Lishe wa halmashauri ya Chalinze,mkoani Pwani, Zainab Waziri ,ametoa rai kwa jamii kuacha kula ovyo bila mpangilio na kuzingatia lishe bora kwa afya ya binadamu ili kujiepusha kupata uzito mkubwa, vitambi na matumbo makubwa kwa akinamama.

Akizungumza wakati wa zoezi la upimaji uzito wa mwili,sukari ,shinikizo la damu na upimaji wa hali ya lishe, kwa watumishi wa halmashauri hiyo ,alisema wameamua kufanya zoezi hilo ikiwa ni maazimio ya kikao cha kamati ya lishe hivyo idara ya afya ikaona itoe elimu kwa watumishi hao na kuwapima.

Zainab alieleza ,wamekuwa wakitoa elimu hiyo katika zahanati,vituo vya afya lakini kundi la watumishi lilisahaulika .

‘”Sisi tunasisitiza ulaji wa chakula mchanganyiko,kuna makundi matano ya chakula ikiwemo nafaka,mizizi na ndizi mbichi,kundi la pili mikunde,tatu mbogamboga,nne mafuta na sukari na kundi la tano ni matunda hivyo unachagua chakula kimoja katika kila kundi”alieleza Zainab.

Nae ofisa mipango wa halmashauri hiyo,Shabani Milao alifafanua,ni vyema utaratibu huo ukawekwa katika kila halmashauri kwani kuna umuhimu watumishi kujua hali zao na kupewa elimu mbalimbali kama zinavyotolewa katika jamii.

Kwa upande wake mtumishi wa halmashauri hiyo,John Mliyambati alisema amepimwa na kuonekana na uzito mkubwa kilo 104 na urefu 179,na ameshauriwa kupungua uzito kwa kupata lishe bora na kufanya mazoezi.

Alieleza,watumishi wamejikuta wakila vyakula vingi bila utaratibu kwakuwa hawafanyikazi ngumu na kula bila mpangilio maalum kulingana na chakula wanachokula hivyo wajitambue kujua afya zao.

Mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze ,dokta Isack Mukungu anaeleza elimu ya lishe inatolewa mara kwa mara kwa jamii,na wana utaratibu wa kuanza kupima virusi vya ukimwi kwenye taasisi mbalimbali na kutoa elimu ili asilimia 90 ya wakazi wa Chalinze wanaoishi na virusi waweze kutambua hali zao.

Alisema kwa sasa Chalinze waliotambua hali zao ambao wapo katika maambuzi ni asilimia 80 hivyo wanataka kufikia malengo ya dunia kwa kufikia asilimia 90 ,ili atakaebainika kupata maambukizi mapya aweze kuanzishiwa dawa za kufubaza virusi.