Home Mchanganyiko KANDEGE- AIPIGIA SALUTE KAMPENI YA ELIMISHA KIBAHA,AAGIZA WAKUU WA WILAYA WENGINE WAIGE...

KANDEGE- AIPIGIA SALUTE KAMPENI YA ELIMISHA KIBAHA,AAGIZA WAKUU WA WILAYA WENGINE WAIGE MFANO

0

*********************************

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

NAIBU Waziri wa TAMISEMI, Josephat Kandege amezindua madarasa 32 na ofisi nne za walimu katika shule za sekondari,yaliyojengwa kupitia kampeni ya ELIMISHA KIBAHA,mkoani Pwani ambayo yatapunguza changamoto iliyokuwepo awali ya mlundikano wa wanafunzi madarasani na yatatumiwa na wanafunzi takriban 900.

Katika hafla hiyo ya kukabidhi madarasa hayo,amewaasa wazazi na walezi kuwapa elimu watoto wao na kuhakikisha wanafuatilia muendendo wa taaluma zao ili baadae watumie fursa ya viwanda vinavyojengwa kwa wingi mkoani humo .

Alisema ELIMISHA KIBAHA ni kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli  za kuhakikisha elimu inatolewa bure kwa kila mwanafuni wa darasa la awali hadi kidato cha nne.

“Haya ni maelekezo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015,ambayo nina ujasiri wa kusema ninyi Kibaha, mmetekeleza,Na nawaagiza wakuu wa wilaya wengine waige mfano wako mkuu wa wilaya ya Kibaha ambae umebuni kampeni hii na kuzaa matunda”alisema Kandege.

Alieleza, hii ni hatua kubwa ,kwani kama mkuu huyo wa wilaya angekaa kusubiri ruzuku ya serikali kuu ama mapato ya halmashauri ndiyo yajenge azma hii isingetimia kwa mwaka mmoja huu.

Kandege alifafanua ,kiuhalisia haiwezekani kuwa na Taifa lililoelimika kama hakuna mazingira bora ya sekta ya elimu ,hali itakayofanya watanzania wawe na ujuzi wa kutosha katika matumizi ya rasilimali zilizopo na fikra chanya za maendeleo.

Hivyo,ubunifu uliofanyika umelenga katika kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

‘”Mkoa wa Pwani umejikita katika uwekeaji wa viwanda ambapo kuna viwanda 47 ambavyo ni vikubwa,vya kati na vidoo vinavyofanyakazi,hii ni fursa kwa wanafunzi kuchangamkia ,kwani bila vijana wetu kuwa na elimu nafasi za kazi za kitaalamu kwenye viwanda hivyo vitachukuliwa na vijana wa mikoa mingine na nje ya nchi.”alisema Kandege. 

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama anasena chimbuko la kampeni ya elimisha Kibaha limetokana na upungufu wa madarasa uliojitokeza mwaka 2019 kutokana na kuongeeka kwa ufaulu mwaka 2018 hali iliyosababisha baadhi ya shule wanafunzi waingie kwa awamu mbili.

“Kufuatia hali hii nilishirikiana na wadau wa maendendeleo ili kuondoa upungufu wa madarasa uliopo  kwa halmashauri ya wilaya madarasa 34 na halmashauri ya Mji madarasa 31”

Mshama ameshukuru ndoto zake kutimia ,na kuweza kujenga madarasa 32 ,na kukusanya kiasi cha sh.milioni 500 kutoka kwa wadau na wananchi.

Kwa upande wake mbunge anaemaliza muda wake, jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka, alieleza katika kampeni hiyo alijitolea kujenga darasa moja na ameahidi kujenga darasa jingine moja,pamoja na mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ameahidi kujenga darasa jingine moja.

Mbunge wa viti maalum wanaomaliza muda wao mkoani Pwani ,Zainab Vullu na Hawa Mchafu wameahidi kutoa mifuko ya saruji 50 kila mmoja.

Mahitaji ya Kampeni ya ELIMISHA KIBAHA  yalikuwa ni kiasi cha sh.bilioni 1.3 kwa ujenzzi wa madarasa 65,viti 3,250 na meza 3,250 na hadi sasa bado kuna upungufu wa madarasa 33 ili kutimiza malengo.